Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Ndugu wanajamvi napenda kushirikiana na nyinyi kwenye hili suala la katiba mpya, kwa jinsi ninavyoona hawa CCM wanavyolazimisha kuhodhi mchakato wa katiba mpya ambayo haikuwa kwenye ilani yao lakini baada ya ushindi wao wa utata hapo mwaka 2010 wakakubali kwa shingo upande kwani walijua wananchi wengi walitaka katiba mpya. Cha ajabu wao hawakuitaka rejea maneno ya C. Kombani na Mwanasheria mkuu wa serekali na hata mizengwe ya wabunge wao wakati wa kujadili kuundwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya jinsi walivyolazimisha wajumbe kama wakuu wa mikoa kuwa ni sehemu ya mabaraza ya katiba na wote tunawajua wakuu wa mikoa wanawakilisha chama gani. Kitu kingine ambacho kinaendelea kunipa mashaka ni pale walipolazimisha rais kuwa na nguvu juu ya uundwaji wa katiba mpya wakati Rais alipaswa kuwa tunda la katiba na sio katiba kuwa tunda la Rais. Hapo ndio ninapoona ni kwa jinsi gani katiba mpya itakavyokosa meno kwani wenzetu wanajua katiba mpya ni kwa ajili ya cha chama cha upinzani kukatamat dola wakati chama cha mapinduzi wanaogopa kutoka madarakani kwani kwa maovu waliyotenda wanajua watafungwa jela. Iwapo katiba ya sasa mambo mengi wanayakiuka watawezaje kufuata hiyo mpya iwapo bado udhaifu tunaouna mpaka leo kwa rais anayetokana na CCM ni kutokutekeleza katiba ya nchi? Kwani mkumbuke CCM hawakutaka katiba mpya na sababu haswa ya wapinzani na wananchi walio wengi kutaka katiba mpya ni kutokana na namna katiba hii ilivyompa madaraka makubwa rais kiasi cha kuyatumia madaraka hayo vibaya. Iweje leo taasisi hiyo hiyo ya urais tunayotaka ipunguziwe madaraka ipewe kitanzi cha kujitundika yenyewe na tena kitanzi chenyewe kilazimishwe kushikwa na chama (CCM) chenye hofu ya katiba mpya yenye kujali maslahi ya wananchi? Ninachokiona hata muundo wa bunge maalumu la katiba mpya litawajaza wabunge wa CCM ambao ama wataihujumu katiba hiyo na kuweka vifungu ambavyo vitaendeleza udhaifu unaipigiwa kelele kwa sasa. Watanzania na nyinyi nawaomba tujadili hili kwa kina na jinsi ya kuhakikisha mchakato huu upite kwenye njia salama kwa ajili ya Tanzania ya miaka 50 mpaka 100 ijayo.