Nabi hana mbinu, anategemea uwezo wa wachezaji tu

Nabi hana mbinu, anategemea uwezo wa wachezaji tu

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kabla ya mechi ya Yanga na Al Hilal niliandika kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa Al Hilal wasicheze mpira wa kushambulia zaidi. Watacheza mpira wa kulinda zaidi kwa hiyo basi watakuwa wengi nyuma na itakuwa vigumu kwa Yanga kupita na mpira.

Nikasema ili Yanga ashinde kuna njia mbili Nabi anatakiwa acheze. Ya kwanza, akubali wapinzani wake wamiliki sana mpira katikati, mana hii itawapa uwezo na nguvu za wao kupanda sana na kuacha mabeki wachache nyuma. Na ya pili ni kuchezesha wachezaji wengi katikati wenye uwezo wa ku piga mbali.

Maana hata wakijilinda sana, wasitegee kuwa mpira utakuwa unafika langoni kwao. Kwa ufupi Al Hilal kwa mpira wao ule tusitegee kuwaona wamefika mbali. Wana mpira wa uoga sana.
 
Ukocha siyo kazi rahisi kama unavyodhan, kuwa na wachezaji bora duniani kwenye timu hiyo pekee haitoshi kuifanya timu kuwa bora na yenye ushindi, there is more than that.

Tatizo la Tanzania kila mtu anataka kuwa kocha, na kila mtu anataka kuwa mchambuzi. Haiwezekani
 
Sasa mbona mnatuchanganya!!!

Mara mseme Nabi hana mbinu anategemea uwezo wa wachezaji na mda mwingine mnadai wachezaji wenyewe wazee wamechoka.

Sasa tuwaeleweje?
🦁Anakushauri nini juu ya mwananchi🤸
 
Eti huyu nae amechambua mechi ambayo Yanga amelala kwa goli moja ugenini hahaha.
 
Timu ni mbovu tu Haina viungo wabunifa ...

Kutana na Liverpool au man city harafu cheza mchezo wa kukaa nyuma uone mvua ya magoli [emoji23]

Timu inayokaa nyuma haiwez kuwa Bora kwa timu inayojua mpira ...

Yanga ni timu mbovu over ....
 
Back
Top Bottom