Nabi: Naiona Yanga ikicheza Nusu Fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2024\2025

Nabi: Naiona Yanga ikicheza Nusu Fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2024\2025

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kocha wa Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi alikuwa hapa nchini kwa siku mbili kisha kufanya vikao na mabosi wa Yanga aliowahi kufanya nao kazi kwa mafanikio lakini amewaambia mabosi hao kuwa anaamini Yanga itacheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Nabi amefanya kikao na Mfadhili wa klabu hiyo, Gharib Said Mohammed, Rais Injinia Hersi Said pamoja na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Anthony Mavunde kisha akawaambia kama ni timu basi msimu huu wanayo.

Kocha huyo raia wa Tunisia amesema kuwa kwa kikosi ambacho Yanga inacho msimu huu ni kizito ambacho sio tu kutinga makundi, lakini kama ikivuka hapo basi itakwenda hadi nusu fainali itategemea na mpinzani gani watakutana naye.

"Nimekutana na viongozi wa Yanga tumekuwa na vikao vizuri vya kifamilia, nilifanya kazi hapa, bado nina maelewano mazuri na viongozi lakini pia wachezaji hata mashabiki na wanachama.

"Nimefurahia kuona kila ninapopita bado watu wanakumbuka kuhusu Nabi, watu wa Yanga, Simba na hata timu nyingine, nimewaambia viongozi kuwa wana timu nzuri sana msimu huu, sitashangaa kama watavuka mbali zaidi ya hatua ya makundi kwa kucheza robo fainali na hata nusu fainali.

"Nadhani ni timu chache zinaweza kuwa na kikosi kizito kama hiki cha Yanga, naamini watafanya vizuri sana hapa ndani na hata Afrika."

Soma Pia: Utabiri: Msimu wa 2024-25, zote Simba na Yanga zitafika fainali za mashindano ya CAF

Aidha Nabi alisema mbali na kuwa na timu bora pia kocha wao Miguel Gamondi mbinu zake zimeongeza ubora mkubwa wa timu hiyo ambayo aliifundisha kwa misimu miwili.

"Sio tu kikosi lakini hata benchi la ufundi ni zuri, nimekutana nao, wana kocha bora sana ambaye falsafa zake zimeipa nguvu zaidi timu hili nalo ni muhimu sana," alisema kocha huyo.

Yanga tayari imeshaweka mguu mmoja ndani kutinga hatua ya mtoano kuwania kufuzu makundi baada ya kushinda ugenini kwa mabao 4-0 dhidi ya Vital'O ya Burundi.
 
Kuna kitu nabi alikiona kwenye yanga kaja kupata darsa kidogo hope kaizer itarudi kuwa team shindani pale SA na hope kaizer family watakubaliana na mabadiliko
 
Kwa sababu amesema yeye au kwa sababu uhalisia upo hivyo?
 
Binafsi naamini Yanga ya Nabi ilikuwa tishio sana kuliko hii ya Gamondi...
Kumbe benchi la ufundi liko vizuri zaidi mwili wa mchezaji ndiyo ngao kuu kuliko hata maajuzi binafsi,(individual skills) unaweza ukawa na mautundu kama huna nguvu utakuwa unadondoka dondoka uwanjani
 
Tatizo ya team za Tanzania zinawekeza kufika robo fainali,nusu fainali wakati wenzao wanawekeza kuchukua ubingwa.
 
Binafsi naamini Yanga ya Nabi ilikuwa tishio sana kuliko hii ya Gamondi...
Kwangu mimi ni Yanga ya Gamondi sababu zangu
1) Yanga ya Gamondi imejipima ubavu na timu za viwango vya juu kwenye CAF ranking ( Al Ahly, Belouizdad, Simba na Mamelodi)
Wakati Nabi alijipima dhidi ya timu zisizokuwa na mwendelezo mzuri katika mashindano ya CAF

2) Aina ya mpira wa Gamondi unavutia zaidi kuliko wa Yanga ya Nabi, mechi ya Uanga dhidi ya Belouizdad ni mechi bora sana kwangu kwa Yanga hadi sasa. Kumfunga Belouizdad goli zile nne hakuna shabiki wa Yanga aliyetarajia
 
Yani nikikumbuka ile mechi najiskiaga hata kulia..
Hakuna mwana Yanga ataisahau Pacome day ile ndio kupindua meza kibabe haitasahaulika kabisa...
Pamoja na mechi ya mtani ya 5 - 1 aah wajameni Yanga 2023 -2024 tuikubali tu
Kwangu mimi ni Yanga ya Gamondi sababu zangu
1) Yanga ya Gamondi imejipima ubavu na timu za viwango vya juu kwenye CAF ranking ( Al Ahly, Belouizdad, Simba na Mamelodi)
Wakati Nabi alijipima dhidi ya timu zisizokuwa na mwendelezo mzuri katika mashindano ya CAF

2) Aina ya mpira wa Gamondi unavutia zaidi kuliko wa Yanga ya Nabi, mechi ya Uanga dhidi ya Belouizdad ni mechi bora sana kwangu kwa Yanga hadi sasa. Kumfunga Belouizdad goli zile nne hakuna shabiki wa Yanga aliyetarajia
 
Yanga ya msimu uliopita ilikuwa nzuri sana alichokosea engineer ni kuifanya super team.

Unapoboresha timu yako nzuri hupaswi kusajili mastaa wengi wapya

Yanga haikupaswa kumsajili, dube hata chama, sababu namba zao hazikuwa na mahitaji mengi. Mzize alikuwepo tayari.. mshambuliaji mmoja tu kama baleke pekee angetosha kumsaidia akitokea benchi. Cha kushangaza wamesajili watu kibao

Yanga ilipaswa kuboresha timu na sio kujenga timu kwa watu wapya

Tazama orlando pirates walichofanya.. timu yao ile ile ya msimu uliopita.. ila katika first 11 yao wamesajili m nigeria mkali mmoja tu kuongeza nguvu..
 
Back
Top Bottom