Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Nabii mashuhuri anayeibukia wa Venezuela, Dionny Báez, amebainisha kuwa
Mungu amemuonesha kuwa rais wa nne wa Kenya. Mwaka 2007, nabii huyo
alibashiri kwamba Kibaki angerejea katika urais na akawa sahihi. Wakati huu,
anaamini kuwa atakuwa sahihi tena. Katika ujumbe wa kinabii alioutoa mnamo
Desemba 2, 2012, uliowekwa Youtube, Báez aliwaambia waumini, jijini Nairobi,
kwamba Mungu amemwonesha kwamba Kenya itampata rais wake ajaye kutoka
Mlima Kenya. Alisema: "Wenye masikio watasikia, Bwana anasema, mtaangalia
mlima mrefu zaidi na kumpata rais wenu ajaye."
Mlima Kenya ulio eneo la Kati ya Kenya kuna watu watatu wanaogombea urais
katika uchaguzi wa mwaka huu, Uhuru Kenyatta, Martha Karua na Peter Kenneth.
Ingawa nabii huyo hakufafanua maelezo yake, wachambuzi wa siasa wanasema
kuwa uhakika wa Martha Karua na Peter Kenneth kushinda haupo kabisa, kwa maana
hawana ushawishi hata katika vitongoji vyao wenyewe. Hii ina maana kwamba
Mtume Báez alikuwa anazungumza juu ya Uhuru Kenyatta kuwa rais wa nne wa Kenya.
Nabii huyo alitabiri kuwepo kwa ghasia nyingine za baada ya uchaguzi, safari hii
zikijumuisha silaha kali zaidi na bunduki kutumika. Hata hivyo alisema kuwa vurugu
zitakuwa na athari ndogo kuliko za 2007/8.
Nakumbuka hapa kwetu, EL ameshatabiriwa na TB Joshua kuwa rais wa tano wa TZ,
na sasa yanatokea huko Kenya, sijui imekaaje hii ya wanaojiita manabii kujiingiza
katika kuwatabiria wanasiasa?...