Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,930
- 2,118
Katika muendelezo wangu wa kuwasakama watani zangu Wapare, leo nitamtambulisha mpare mmoja aliyekuwa kiboko ya wapare wenzie.
Mpare huyu alijiita Nabii Elia (Eliya) wa upareni.
Mtu huyu alikuwa ni wa kutokea pande za Usangi ila akahamia Same Kisiawani kwenye Milima pembeni ya njia ya kuelekea Kighare au hata Mahore huko.
Kisiwani ni sehemu ya mlimani iliyo tambarare ukiwa unaelekea Gonja.
Mabasi ya kampuni ya PHIBA huwa yanaelekea Gonja.
Huyu jamaa aliyejiita nabii inasadikiwa alikuwa mchawi wa kupindukia na aliweza kuwaafanya waumini wake wahamie kwake wakiwa na familia zao. Wengi wao waliamini alikuwa ni nabii kama alivyo Gwajima.
Basi baada ya kuhamia kwake wanaume wote walikuwa wakifanya kazi za shamba na kuchunga mifugo (alikuwa akimiliki mashamba makubwa sana). Hata hivyo wanawake na wasichana walibaki kwa nabii kwa ajili ya kupatiwa "semina".
Semina hizi walikuwa wakiingia kwa zamu kwa nabii mtu mmoja mmoja. Huko chumbani nabii Elia aliwatumia kingono wanawake hao kwa kadiri alivyopenda. Kwa maneno mengine alikuwa akishiriki vitendo vya uzinzi kwa mama na mabinti zao na hakuna aliyekuwa anaweza kufanya lolote zaidi ya kushukuru.
Endapo mwanaume angekuja akiwa na viatu vizuri basi ikiwa vitachakaa angenunuliwa viatu vya matairi (masendeu) na nabii. Wanawake wao walikuwa wakishonewa sare 2 tu na wote walivaa nguo za kufanana.
Ilikuwa ni marufuku kutoka nje ya geti bila kuwa chini ya usimamizi na ikiwa mtu angetoka basi angechapwa viboko hata mbele ya mke na watoto wake.
Nabii huyu aliwaambia watu wake kuwa ikitokea akafariki basi wasimzike kwani atafufuka baada ya siku 3. (nimekumbua kisa hiki kwa kuwa leo ni Pasaka).
Kweli baada ya muda mrefu (sikumbuki mwaka) Nabii huyu alifariki na kama alivyoagiza, waumini wake hawakumzika na walikaa na maiti kwa siku 3 ndani. Hata hivyo harufu ya maiti ilizidi kuwa kali na wakajua wazi hawezi kufufuka hivyo ikabidi wamzike.
Hadi sasa baadhi ya wanawake aliokuwa akizini nao bado wapo wanaishi kwenye eneo lake na ndoa nyingi zilivunjika kila mmoja akashika lake.
Pamoja na kuwa watu wa Usangi ni wavivu sana lakini huyu Msangi aliwaweza sana wapare wenzie na kuwafanya watumwa huku akiwakula wake zao......