Hizo pesa za kugawagawa ilhali washirika wake wengi ni makapuku, na mali kama hayo magari huyo nabii wako anatoa wapi? au naye ndiyo wale wale wanaosemekana kuwa wadau wa mackenzie?
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mathayo 7:15
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
Mathayo 24:24
Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.