LGE2024 Nachingwea: Asilimia 99 ya wagombea waliowekwa na CHADEMA waenguliwa kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Uchafuzi wa Serikali Za Mitaa bado unaendelea.

Hivi karibuni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Wilaya ya Nachingwea kimeeleza kusikitishwa na hatua ya kuenguliwa kwa wagombea wake kuelekea uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa, licha ya wagombea hao kuwa na sifa stahiki.

Akiongea na waandishi wa habari, Katibu wa CHADEMA wilayani humo, Ramadhani Hamis kuwa chama hicho kilisimamisha wagombea katika vijiji 80 kati ya vijiji 127 vilivyopo katika wilaya hiyo, pamoja na wagombea katika vitongoji 271 na wajumbe wa serikali za mitaa, na kufanya idadi ya jumla ya wagombea kufikia 1,524.

Soma pia: Je, kuenguliwa wagombea wa CHADEMA nani alaumiwe kati ya Mbowe, Lissu au Rais Samia?

Hata hivyo, kati ya vijiji 80 walikosimamisha wagombea, ni vijiji 9 pekee vilivyopitishwa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.

Mashujaa.jpg

Aidha amesema kwenye vijiji themanini vijiji tisa ndivyo vilivyoteuliwa kushiriki uchaguzi na kwenye vitongoji 271 vitongoji 30 ndivyo vimeteuliwa na zaidi ya asilimia 99 wameenguliwa kwa upande wajumbe wa serikali za vijiji na mitaa 2 ndiyo imeteuliwa kati ya mitaa kumi na sita kwenye vitongoji vya mamlaka ya mji mdogo waliosimamisha wagombea wao.

Msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Kawawa Chionda alitoa ufafananuzi kwa njia ya simu akisema kuwa vyama vyenye malalamiko yoyote kuhusu zoezi la uchaguzi kufuata njia rasmi kwa kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi kupitia ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi ili kushughulikiwa kisheria.
 
Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1 (1).png
    Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1 (1).png
    420.8 KB · Views: 5
  • 20240907_095744 (1).jpg
    20240907_095744 (1).jpg
    116.1 KB · Views: 4
  • IMG-20200726-WA0000.jpg
    IMG-20200726-WA0000.jpg
    43.7 KB · Views: 4
  • 5810871-156c33252d331784831e630b50148deb.mp4
    2 MB
  • 5811523-6041f5af6e2b5c7600d07027005d6658.mp4
    3.7 MB
Back
Top Bottom