LGE2024 Nachingwea: Diwani Veronika Makotha awahimiza wanawake na vijana kujitokeza kujiandikisha na kugombea nafasi za uongozi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Nachingwea: Diwani Veronika Makotha awahimiza wanawake na vijana kujitokeza kujiandikisha na kugombea nafasi za uongozi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Vijana na wanawake msituangushe uchaguzi huu, ruacge kulalamika, tuingie kwenye uongozi na kuleta mabadadiliko tunayoyataka.

Hata kama wazee mifuko imetuna, kama tukisimama imara na kuchagua viongozi waliobora rushwa haitapata nafasi ya kuamua kiongozi bora, malalamiko tuyaache kwenye chaguzi zilizopita, muda huu uwe wa kufanya kweli.

====

Tarehe 16/10/2024, Diwani viti maalum kata ya Mpiruka, Veronica Makotha, alifanya mkutano muhimu katika kijiji cha Mkumba. Lengo la mkutano huo lilikuwa kuhamasisha uandikishaji katika daftari la waakazi na kuchangamkia fursa za mikopo kwa vijana.

Katika mkutano huo, Veronica aliwasisitizia vijana umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la mkazi, akisema kuwa ni hatua muhimu katika uchaguzi na katika kuomba nafasi mbalimbali za uongozi. "Siku zilibaki, tutumie fursa hii kwa uaminifu," alisema. Aliweka wazi kuwa kujiandikisha kutawasaidia vijana kutambulika katika jamii zao.

Pia soma:
LGE2024 - Lindi: Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete ajiandikisha kwenye daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Veronica alikumbusha kwamba wanawake wamekuwa nyuma katika kujiandikisha, na akatoa wito kwao kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika uchaguzi na kugombea nafasi za uongozi. "Umefika wakati wanawake wawe daraja kwa uongozi, lazima tujiandikishe na tugombee," alisisitiza.

Mafisa maendeleo ya jamii pia walihimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuchangamkia mikopo ya 10% inayotolewa kwa lengo la kuwasaidia kiuchumi. Wananchi walionyesha ari kubwa ya kushiriki uchaguzi na fursa za mikopo, wakionesha utayari wa kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Mkutano huu umethibitisha kuwa wananchi wa Mkumba wako tayari kuchangia maendeleo yao na kuchangamkia fursa zilizopo.


Kupata matukio yote ya mkoa huu soma: Lindi: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
 
Mnaochukua form za Uchaguzi msisahau kabisa kutafuta waganga wakali wa kuwasaidia michezo yenu.

Hapa kuna kurogwa ukapooza, ukapindishwa mdomo, ukasahaulishwa kila kitu hadi kufa kabisa.

Msiseme sikusema.
 
Back
Top Bottom