Nachukia mijusi hata kinyesi chake, nikiona nashindwa hata kula

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Yaani nachukia mijusi balaa, hata nikiona kinyeshi chake ndani tu mfano bafuni aisee huwa siogi. Nikiona hata wakati nakula huwa nashindwa kula hata chooni natamani kukimbia.

Kinyesi cha wanyama wote nashika, ng'ombe etc, maana before nilikuwa mfugaji. Siogopi hata nyoka wala chochote, except mavi ya mjusi.

Kitandani ndio nitahama kabisa hasa kipindi cha mvua nakumbuka mwaka jana mkoani masika nilienda familia moja huko nikakaribishwa na pa kulala sasa kilikuwa kipindi cha mvua, aisee chumba safi ila nilivyokuta kinyesi cha mjusi tu kitandani yaani niliondoka na mabegi yangu nikaenda kulala guest house.

Nachukia sana kinyesi cha mjusi, siwezi shika kwa mikono yangu kabisa yaani ukiniambia hata nibebe na mikono unipe pesa sitaweza.

Yangekua dawa ya ugonjwa nambiwe ninywe nipone yaani sitoweza ni bora nife tu, yaani sijui kwanini nina allergy na mjusi na kinyesi chake mimi huhisi kinyaa sana.
 
Sasa utaweza kupambana na U.S militants kama kinyesi cha mjusi kinakutepetesha?
.
Watu tunashika mavi ya ng'ombe na hatunawi tunashika manumbu tunakula.
Kwenye togwa hatutoi sungusungu tunawanywa ohoooo utakufa mapema
 
Sasa utaweza kupambana na U.S militants kama kinyesi cha mjusi kinakutepetesha?
.
Watu tunashika mavi ya ng'ombe na hatunawi tunashika manumbu tunakula.
Kwenye togwa hatutoi sungusungu tunawanywa ohoooo utakufa mapema
Mavi ya ngombe nashikaga mkuu na nimezoea ila mjusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kua na allergy na amphibia ambao Wana rough skin Hata me nnayo Mana hawapendezi kukaanao Hata kuwaona ila.my dear nyoka ni mzuri Ana ngozi nyororo[emoji3059]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…