NACTE Guide BOOK ya Diploma and Certificate za Vyuo Vikuu

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
7,602
Reaction score
7,332
Juzi juzi niliandika haya baada ya kusoma tangazo la udahili la UDOM
kama za Diploma hutaziona mahali popote isipokuwa kwenye tangazo hili-hazina guide book.

Sasa leo nimekutana "THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES OFFERED BY UNIVERSITIES ADMISSION GUIDEBOOK FOR 2020/2021" kwenye web page ya NACTE ambayo haikuwa na maelezo yeyote ukizingatia ni mara ya kwanza wanatoa document hii. Nikaangalia UDOM nikakuta mle ndani wana Certificate programs 7 na Diploma programs 20. Najiuliza kwa vijana wetu wafuate ipi-ya NACTE au UDOM . Sikutegemea kamazitakuwa tofauti.
Nikazama ndani kuangalia vigezo vilivyowekwa ili mtu adahiliwe na hapa nikagundua kuna tatizo, kwa mfano Diploma ya Information and Technology ambayo ni miaka 2 wameandika " Holder of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with Four (4) passes in non-religious subjects including pass D in English subjects" Lakini vigezo hivi ni vya Certificate course au Diploma course ya miaka 3. Pia utaona vigezo vyao vimewaacha wale form 6 kabisa kwa course hii. Kwa staili hii ndugu zangu tutafika? NACTE na UDOM wanatakiwa waliweke sawa.
Hata hivyo nawapongeza NACTE kwa kuanzisha hii guide book itasaidia wanao omba certificates na diploma vyuo vikuu lakini inahitaji marekebisho ili iwe msaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…