Wadau tufafanulie kuhusu hili.Sifa inayojulikana kwa wanaoomba Elimu ya juu ni Kidato cha Sita,Kidato cha Nne na Stashahada ya B grade.Lakini kuna Watu niliosoma nao wamepitishwa na NACTE kwa Elimu ya juu wakiwa na Kidato cha Nne na Stashahada ya C PASS.Tueleni kama viwango vimebadilika tuchukue fomu kwa kuwa mwanzo tulisita kwa kufuata matangazo ya Vyuo husika.Wana JF wenye ufahamu wa hili na NACTE mtuelimishe.
Mimi ni Kidato cha Nne na Stashahada ya daraja C (PASS)Kabla sijakusaidia ufafanuzi, naomba kujua wewe una sifa gani kati ya hizo ulizotutajia.
Vinginevyo itakuwa vigumu kukupatia msaada utakaokufaa.
Kwasababu mtu wa kidato cha sita, mwenye mchundo (FTC) na mwenye diploma wanatofautiana alama za kujiunga na elimu ya juu,
wewe uko kundi gani?