Wakati huu wa sayansi na teknolojia, kazi zimerahisishwa sana.
Inashangaza kuona baadhi ya taasisi za serikali zinashindwa kwenda haraka katika utendaji kazi kiasi cha kuharibu ratiba za maendeleo ya wananchi pasipo sababu ya msingi.
Nacte wamepokea matokeo ya wahitimu wa NTA level 6, lakini wamekaa nayo kimya huku wakijua kuna baadhi ya wahitimu wanataka uthibitisho wa matokeo hayo ili kuomba nafasi kuendelea na masomo yao vyuo sambamba na kuombea mikopo ya kuendelea na masomo.
Kuthibitisha matokeo si kazi ya kusubiri hadi wakati wa kiangazi wala masika. Ni wakati wowote yanapopelekwa kwako. Wanakaa na matokeo zaidi ya wiki huku wakijua muda wa kuomba mkopo unaisha tarehe 31 Agosti na hadi leo ni juma moja tu limebaki.
Nacte, mnatukomoa?