KERO NACTVET hawaoneshi ushirikiano kwa wanafunzi wanoomba AVN number kwa ajili ya matumizi ya kuomba mikopo na vyuo

KERO NACTVET hawaoneshi ushirikiano kwa wanafunzi wanoomba AVN number kwa ajili ya matumizi ya kuomba mikopo na vyuo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Joseph41

Member
Joined
Mar 21, 2024
Posts
16
Reaction score
5
Ikiwa Leo ni siku ya nne, najaribu kuingia kwenye system ya "NACTVET" Kuomba "AVN NUMBER" lakini sifanikiwi licha ya kuwa nimejisajili, ila system haijanipa nafasi ya kutengeneza password, na hata siwezi kuingia kabisa, na mbaya zaidi mfumo unload tu Wala hata haufunguki.

Ikiwa zimebakia siku tatu tu kufungwa Kwa dirisha la application vyuoni, na mkopo pia hivi karibuni watafunga, lakini NACTVET hawaoneshi ushirikiano kabisa.

Licha ya kuwa wameweka namba za mawasiliano lakini haipatikani na baadhi hazipokelewi hata moja, na tukituna notifications kwenye email yao, hawatusaidii!

NB: Ni vyema wakwasaidia wanafunzi wanaopata changamoto kama hizo na baadhi, kwani hii inasababisha kurudisha maendeleo ya wengi nyuma, na taifa Kwa ujumla.
 
Mfumo wa NACTVET wa kuomba AVN Number unashida kubwa na wahusika (NACTE) hawalichukulii maanani hilo tatizo maana raia wengi watakosa kuomba vyuo hichi kipindi sababu AVN Number ni muhimu sana katika maombi ya vyuo kwa wale waliohitimu DIPLOMA. Deadline ya Maombi ya chuo ni Tarehe 10/08/2024. Nawaombeni jukwaa la JF mlifatilie hili jambo ili sisi ambao tunataka kuwa wanafunzi tusaidiwe kutatuliwa hii changamoto.

Binafsi nilifuatilia kupata tatuzi la hii shida offisini NACTVET HQ (Mikocheni, Dar es Salaam) ila sikufanikiwa kutatuliwa hii shida na nilikutana na wanafunzi wengi wenye hii shida ambao kwa wiki nzima wamekuwa wakifatilia kutatuliwa hili tatizo bila mafanikio yeyote.
 
Samahana naomba kuuliza jamani, ivi sheria ya mwanafunzi wa bachelor degree mwaka wa pili kutoruhusiwa kucarry somo kwenda nalo mwaka wa tatu ni vyuo vyote au ni chuo changu tu ? (Maana hii nactvet, nashindwa kuelewa)
Na je nawezaje kupata pdf ya hiyo sheria ya v
Naomba msaada.
 
Back
Top Bottom