Mrekebishaji
Senior Member
- Mar 19, 2009
- 168
- 63
Nilikuwa nisafiri kwa shirika fulani la ndege toka Dar kwenda Nairobi. Nikaahirisha safari. nikatoa taarifa airport mahali nilipolipia na kuwaambia nimeshindwa kusafiri, wakasema tiket itakuwa wazi mpaka mimi nikithibitisha kuwa nasafiri lini ndio wataweka tarehe hiyo. ilikuwa June 28, 2012. kesho yake, baada ya kuona sitasafiri tena nikaenda ofisini kwao na kujaza form ya kuomba kurudishiwa fedha. Niliambiwa huchukua wiki tatu na nilijua hivyo. zikapita wiki tatu, kila nilipofuatilia naambiwa mhasibu hayupo, baada ya muda mrefu kupita, mara mhasibu akasema claim yangu imekwama, madai yangu yamekuwa labelled 'Void'. Baada ya kufuatilia nikaambiwa kuwa yule mtu wa airport aliandika kuwa mimi nilirudishiwa fedha palepale. KITU AMBACHO SI KWELI. nikaambiwa nifuatilie kwa Finance Manager wao. nilikutana nae, akasema ni nimpe maelezo ilivyokuwa. Akasema nimtumie email maelezo yangu. then akanijibu kuwa niseme lini nitaenda nikutane na boss wao mwingine. Siku nikaenda, nikawekwa 'KITIMOTO' katikati ya watu kama nane hivi. wakanihoji, kwa ufupi ni kama mtuhumiwa. Nikaeleza ukweli kuwa mimi sikurudishiwa fedha, lakini pia nilishangaa sana shirika kubwa, eti aiport mtu akighairi safari wanaweza kurudisha fedha palepale na staff wao anasema mimi alinirudishia, nikasema ina maana hamna sehemu ya mtu anaposaini kuwa amerudishiwa wakasema hawafanyi hivyo,ila wanakati ticket kwenye system basi. NIKASHAANGA SAAAAANA. Haihitaji uhasibu kujua hapo ni kosa huwezi kuwa na mfumo unarudisha fedha bila mtu kusaini kuwa amepokea. wakakiri kosa. Niliwaambiwa hiyo itatoa fursa kwa wafanyakazi wao kufanya utapeli kuwa wamewarudishia fedha watu kumbe si kweli, a mteja hawezi kuangalia computer yao na kuona umeandikiwa umelipwa kumbe si kweli. Wakasema itabidi waombe camera za aiport ili zionyeshe kama nilirudishiwa fedha au la. Baada ya kama wiki tatu nikapigiwa simu na watu wa 'usalama' wao wakinihoji. Lakini mpaka sasa ni kama wiki tatu zimepita tena kimya. Nimeandika email mbili sijajibiwa. Zaidi ya laki tano. UKWELI ni kuwa sasa imepita miezi minne na sijui hatma yangu. Naomba ufafanuzi wa kisheria. Moja nimetuhumiwa kuwa ni kama tapeli wakati si kweli, tunangoja ushauri. lakini pia fedha yangu kukaa huko kwa zaidi ya miezi 4 ni hasara kubwa, na wote tunajua. USHAURI WENU PLSE.