Nadhani kauli ya Ali Kiba imetufanya Watanzania tukose tuzo MTVMAMA2016

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
183


Kwanza nianze kuwapongeza Wasanii wa TANZANİA ambao walifanikiwa kuingia katika kuwania tuzo za [HASHTAG]#MTVmama2016[/HASHTAG] kwa kuwa wamezidi kuizilishia Afrika kwamba sasa muziki wetu wa Tanzania Umepiga hatua kwa kiasi kikubwa sana kutoka kuwakilishwa na msanii mmoja mpaka wasanii zaidi ya watano ni bonge la hatua sana.

Pili napenda kumpongeza [HASHTAG]#Diamondplatinumz[/HASHTAG] kwa kuzidi kuwa ambassador namba moja wa muziki wa bongofleva ndio hata anbayo imesababisha leo hii tunawakilishwa na wasanii zaidi ya watano #BİGUP DİAMOND

Tatu kwa maoni yangu japo sıtaki nieleweke vibaya lakini ni katika kuhakikidha safari ijayo kwenye mashindano wasanii wetu wajifunze kuwa kitu kimoja hii itatusaidia kuzidi kufanya vizuri, Mimi naona kauli aliyoitoa Alikiba kuhusiana na meneja wa diamond akidai alimfanyia vitendo şi vya kiungwana ni miongoni mwa sababu kubwa iliyopelekea #TZ ikose tuzo yoyote.

Nne Kauli aliyoitoa #ALİKİBA ilijenga taswira kwa wapigaji kura wa afrika mashariki kwamba wasanii wa TZ hawana UNİTY mbaya zaidi ilitoka kipindi ambacho tulikuwa tukihitajika kupiga kura kwa sana lakini mambo yakawa Tofauti mwisho wa siku kila Timu ilikuwa ikimsapoti msanii wake pekee.

Tano hili lilitokea liwe funzo kwa wasanii wetu lakini natoa wito kwa wasanii na sisi mashabiki tujifunze kuungansha nguvu zetu na kumaliza [HASHTAG]#BEEF[/HASHTAG] pindi inapofika wakati wa mashindano ya kimataifa pia wasanii wetu muanze kutafuta Collabo zenye kuwajenga kimuziki ila [HASHTAG]#Alikiba[/HASHTAG] punguza collabo za ndani tuletee za nje, Diamond rudisha mahusiano yako na wasanii wakubwa wenzio kama #WİZKİD #DAVİDO

Sita kuhusu kushindwa kwa wasanii wengine kama [HASHTAG]#VANESA[/HASHTAG] [HASHTAG]#RAYMOND[/HASHTAG] [HASHTAG]#NAVYKENZO[/HASHTAG] hawa bado wachanga na hawajajitangaza vizuri kinataifa ukilinganisha na waliokuwa washindani wao ongezeni bidii mwakani tuchukue

[HASHTAG]#kijanamzalendo[/HASHTAG] [HASHTAG]#ilovetz[/HASHTAG]. [HASHTAG]#maoniyangu[/HASHTAG]
 
Muziki Tanzania umekufa rasmi

Tusitafute wa kumlaumu wakati ukweli upo wazi,
Wengi tulijifanya kutengeneza timu tukasahau mziki hauna kombe

Sasa tuzo za kimataifa asipochukua Diamond na wale Wachafu wa Wadale basi Tanzania imekosa,


Bora hata Mkwere alijua nini huwa kinafanyika wapi pakiwaje

Lakini hili dudu la sasa hivi ni janga 120%
 
Acheni kumlaumu kiba Wa Nigeria wametuzidi kimuziki diamond hafiki hata robo kwa wizkid anayejulikana Africa, Same to Vanessa hakuti kiwango cha Yemi, pia rayvann Ku compete na Techno mzee wa duro napo ni sawa na Ku compare mbingu na ardhi, hao Yamoto hata cjui wanajulikana hata Sudani. Wasanii wajipange tu wanaija na south level nyingine
 
Mtoa mada mwambie aliekutuma hujatukuta, uje siku nyingine.

Kweli mbaazi ikikosa maua husingizia jua, kila msanii kakosa tuzo kwa sababu zake, kati ya sababu ilomfelisha mondi ni kukopy video za wenzie kwenye kidogodogo pale alichemka sana n hata mwenyewe alijistukia akaamua kutoa salome fasta fasta ili asikose tuzo bt alisahau kila baya moja hufuta mema elf na ilikua too late ajipange upya asubr mwakan, mwachen kiba wa watu apumue
 
sawa huyo kiba anaeza kuwa alikosea kwa hyo kaul unayosema...ila ww ndo m'baya zaid maana unazidi kumwagia petrol moto ulioanza kuzmika!!!pia mbna umeandika kimahaba sana yan inakuwa kama umetumwa na mtu anaefaidika kwa tofaut zilizopo kat ya kiba na mond!
 
hivi MacMugaa anajua swaiba wake nae ameeda RSA na anarud bila kitu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Toa remix bwana macMuga
 
yani kwa kukosa tuzo mwaka huu basi umekufa,hii ni changamoto kwa wasanii kufanya vizuri zaidi,na sidhani kama watakuwa na wamawazo kama yako kwamba muziki wa Tz umekufa


 
Iv ni wadogo kwa kiwwngo vp tuzo zingine wanazoshinda?hao waija hawashirik?
 
Kwa hiyo ukikosa Tuzo unatafuta wa kumlaumu? Kwani nchi zote zimepata Tuzo? Acha mihemko wewe.
 
Na MA team uchwara ya watu... Mpaka kimataifa watu wanaleta mateamz sijui nini kimetulaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…