Nadhani kuna mambo ya kibiblia huwa yanajirudia rudia katika vipindi mbali mbali, in a small way

Nadhani kuna mambo ya kibiblia huwa yanajirudia rudia katika vipindi mbali mbali, in a small way

z12f

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
704
Reaction score
572
Nadhani mambo ya kibiblia huwa yanajirudia rudia katika vipindi mbali mbali, na katika maeneo mbali mbali in a small way.

Story ya Samson na Delilah inaweza kujirudia in a small way kwenye maisha ya watu katika vipindi tofauti vya kihistoria.

Kwenye Ufunuo 13 (Revelation 13), kuna mamlaka inayowapiga vita na kuwachosha watakatifu na kufikiri kubadilisha majira na sheria. Na inaongea maneno makubwa dhidi ya Mungu na watakatifu wake. Watu wote wataiabudu hii mamlaka kasoro watakatifu. Mamlaka hii hii iko kwenye kitabu cha Daniel ikiukanyaga ukweli ardhini (Neno la Mungu wa Israel). Mamlaka hii ilipewa kipindi maalum cha kutawala cha miaka 1,260. Baadae ikaja mamlaka nyingine ya Image of the Beast au False Prophet, aliekuwa na pembe mbili za kondoo lakini aliongea kama joka.
Watakatifu waliishinda hii mamlaka kwa damu ya Mwanakondoo na kwakutoa ushuhuda wa kweli.

Je unajua nchi yeyote inayofanana kidogo na hii scenario in a small way?

Of course, nchi hiyo (au hizo) bado hazijafika huko (hata in a small way), ni vizuri tu wajitahidi wasifike huko.

Utawala mzuri utakua na tabia zifuatazo:

1) Haki itashamiri. Watu wote wa makabila yote na dini zote watashamiri.

2) Cylinder zote za engine ya kiuchumi zitafanya kazi vizuri. Kilimo, misitu, mazingira, uvuvi, utalii, mifugo, biashara, viwanda, madini, nishati, gesi na mafuta etc.

3) Watanzania wengi sana watakua na elimu nzuri ya msingi, zaidi ya nusu ya watanzania watakua na elimu nzuri ya form six na atalirudisha darasa la nane.

4) Mikoa yote na makundi yote yatapiga hatua nzuri za kimaendeleo na kimaisha. Hatachukia jamii yoyote, mkoa wowote au dini yoyote.

5) Atajenga miundo mbinu yenye tija na isio na gharama kubwa sana. Runways za viwanja vya kimataifa vya ndege zitakua between 4 kms and 5 kms. Atajenga barabara ya kiwango cha lami itakayo unganisha Karatu na Mwadui moja kwa moja kupitia kaskazini mwa ziwa Eyasi. Atajenga barabara ya kiwango cha lami itakayo unganisha Lindi na Morogoro moja kwa moja kupitia Mbuga ya Selous. Atajenga kiwanja cha ndege karibia na Songosongo ili kikuze utalii wa Selous na uwekezaji kwenye gesi. Atajenga bandari Rukwa kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika. Atarefusha runway ya airport ya Arusha.

6) Atatetea ustawi wa Tanzania kwenye nyanja za kimataifa na atakua na mahusiano mazuri na majirani wema wa Tanzania.

7) Ataiondoa Tanzania kutoka kwenye mahusiano tegemezi ya kisiasa na kiuchumi. Atatetea national sovereignty and self-determination na ataiondoa Tanzania kutoka kwenye makucha ya madeni ya nje hususan madeni ya kibiashara yenye riba kubwa.

8) Atachukia na kupiga vita corruption na ata promote good governance, human rights na ataheshimu legitimate private property rights. Ataheshimu pia tax payers’ and community property rights (matumizi mazuri ya kodi na rasilimali za jamii).

Ataweka katiba ambayo Rais hatakua na uwezo wa kulivunja bunge kabla ya uhai wa miaka mitano ya bunge kuisha. Bunge nalo halitakua na uwezo wa kumfukuza Rais. Ikitokea mvutano kati ya hao wawili basi popular referendum ya wananchi itaamua yupi aachie ngazi. Na atakae baki atatawala mpaka hio miaka yake mitano iishe. Ataheshimu uhuru wa mahakama. Ataheshimu na kuimarisha na kuboresha decentralisation na serikali za mitaa.

9) Atambue kuna mizunguko mikuu na mabadiliko makuu ya majira na nyakati ambayo huwa yanatokea kwenye universe, hapa duniani na Tanzania. Utawala wa Mjerumani pamoja na Muingereza ulikua miaka 70 (pale Tanganyika ilipokua official colony la mjerumani, pale serikali ya ujerumani ilipo take over from German East African company hadi Tanganyika ilipopata uhuru kutoka kwa muingereza).

Concept ya miaka 70 utaiona kwenye kitabu cha Jeremia ambapo mataifa ya wakati ule yalitakiwa kutumikia ufalme wa Babeli wa wakati ule kwa miaka 70. Miaka ya late 1950s na early 1960s winds of change zilivuma zilizopelekea kupatikana kwa uhuru wanchi nyingi za afrika. Vile vile miaka sabini baada ya uhuru inaishia 2031. Sasa sijui waafrika watarudishwa kwenye ukoloni na utumwa au watapungua sana au sijui labda watastawi zaidi na kuwa na uhuru zaidi. Au labda kundi jipya la utawala ambalo halijawahi kutawala litaingia madarakani nchini Tanzania kutoka ndani au nje ya existing political power structure.

Miaka 2000 baada ya Stephen kupigwa mawe inaishia around 2035, hii itatimiza miaka 2000 ya injili kwenda kwa mataifa na kanisa kuwa mtunzaji mkuu wa injili. From Adam hadi Abraham (around 2000 years) patriachs ndio walikua watunzaji wa tumaini la injili. From Abraham hadi Yesu (around 2000 years) Abraham, Isaac, Jacob na uzao wao (Taifa la Israel la wakati ule) ndio walikua custodian wa tumaini la injili. So huenda kuna mabadiliko ya majira na nyakati (a change in times and seasons) yatatokea mitaa ya miaka ya 2030-2040. Wakati huo dunia itakua na miaka around 6034-6044. Dunia itakua iko extra time kwa miaka 34-44 baada ya kumaliza miaka 6000 ya uwepo wake. Uwezekano upo wa extra time kuendelea mpaka 6666.

Ni muhimu sana kwa Watanzania kuijua injili ya kweli kabisa (bila kujali madhehebu yao) hata kama kwenye maisha yao halisi watakua hawaifuati kikamilifu.

1) Yesu Kristo kwa kiebrania ni Yahushua Mashiah. Yahushua maana yake ni YAHWEH is Salvation. YAHWEH ni Mungu wa Abraham, Isaac na Jacob.

2) Yesu alizaliwa during the Feast of Tabernacles.

3) Siku takatifu ya kikweli kweli kabisa inaanza Ijumaa jioni (jua linapozama) na inaisha Jumamosi jioni (jua linapozama) (Seventh day Sabbath). Avoid kufanya dhambi muda huu (of course tunatakiwa tu avoid kufanya dhambi muda wote).

4) Waafrika weusi ni watoto wa Noah kupitia Ham kupitia Mizraim, Cush and Phut.

5) Ni vizuri watu wote wa avoid pride, arrogance, malice, hatred and envy.

Mafanikio ya kidunia yatatokana na:

1) Ku successfully participate in the major means of production, distribution and exchange in the economy in an atmosphere of low inequality.

2) Ku successfully participate in the neo-liberal global economy.

3) Kushirikiana vizuri na watu wengine, na kuavoid mahusiano yanayoleta hasara.

4) Majority ya Watanzania wajitahidi kupata elimu ya form 6 na kuendelea.

5) Kuishi a healthy lifestyle (including exercising), itakayowawezesha kuishi kwa muda mrefu huku wakiwa na afya njema kabisa.

Bwana Yesu Kristo anapenda mataifa yote yawe na nuru ya injili ya kweli. Anapenda kuwa na wafuasi kwenye mahema yote ya Shem, Ham na Japheth.

Ni vizuri watanzania waishi vizuri na kushirikiana vizuri (kiuadilifu) katika nyanja mbali mbali kama ambavyo wamekua wakifanya kwa muda mrefu.

Asante
 
Msomaji anaweza kulink in a secular way. Kwa mfano mamlaka ya Ufunuo 13 inafikiri kubadilisha majira na sheria ya Mungu. Mamlaka ya kisiasa ya nchi husika inafikiri kubadilisha katiba ya nchi in an unhelpful direction. Etc.

Hii inasaidia kutoa a mild behind the scenes perspective in the spiritual world of what is happening in the physical political world. Itasaidia watu kujua majira na nyakati ili wasurvive na kufanikiwa vizuri kwenye kipindi hichi, na wasipoteze muda wao ku protest bila kujua kiini cha wanacho kiprotest.
 
Umeandika kitu kikubwa sana na kigumu mno. Mungu atukuzwe.
 
Back
Top Bottom