Nadhani muda umefika viwanja vilivyo chini ya CCM virejeshwe kwa wananchi visimamiwe na serikali

Nadhani muda umefika viwanja vilivyo chini ya CCM virejeshwe kwa wananchi visimamiwe na serikali

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Sina budi kupongeza juhudi za serikali awamu ya kwanza na ya pili kwa maamuzi yao ya kuthamini michezo na kuweza kuhamasisha ujenzi wa viwanja vya michezo karibu katika mikoa yote.

Ujenzi huu ulitokana na michango ya wananchi wote bila kujali itikadi au kama ni mwanachama wa CCM au la,kwani kulikuwa na chama kimoja tu.

Mtindo wa ujenzi wa viwanja hivi ulikuwa kwa mfumo wa michango kama tulivyokuwa tunachangia ujenzi wa mashule ya kata wakati wa Mkapa na Jk.

Kutokana na nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi,CCM waliona vyema kujimilikisha viwanja hivyo na hasa kwa vile waliviita majina ya mfano CCM Kirumba.

Lakini kusema kweli, CCM imeshindwa kuvihudumia na sasa serikali inabidi ndiyo iingilie kati.Ijapo ni jambo gumu lakini kwa waungwana linawezekana. Kwani hivi vyama vya siasa ni vya watu wachache tu.Wananchi wengi hawajihusishi na vyama vya siasa.

Kwa mtu mzalendo, muungwana ataliona jambo hili. Raslimali za nchi, zisigawanwe kwa misingi ya makundi ya kisiasa au itikadi fulani,
Ili kila mtu afaidike sawa.

Ni muhimu kuvirudisha serikalini viwanja hivi sasa.Muda muafaka ndio huu.Na serikali inaweza kuvikabidhi kwa shirika la nyumba la taifa.

Hayo ni maoni yangu huru. Mimi sina itikadi ya chama chochote.Kuna watu humu huwa huwa wanafikiri kila mwananchi ni mfuasi wa chama fulani.Ninaongea kama mwanamichezo,ninayeona umuhimu wa serikali sasa kuwa na viwanja vyake yenyewe na Sio chama fulani cha siasa .
 
Kwanza pole kwa kukosa usingizi, pili pole kwa kilichokukosesha usingizi,tatu pole kwa uwanja uliouona na hadi kuja hapa kutoa maoni.
Viwanja hivi wakati vinajengwa vilikuwa vinajengwa chini ya umoja wa wazazi Tanzania ambayo ni jumuiya hai cha CCM.

Kama ilovyo katika shule zao za umoja huo, Chama cha CCM kupitia katibu mkuu wa jumuiya hii wanaweza wakakutana na wana CCM wengine viongozi wa kichama na jumuiya zake kujadili kuona wauze au laa?

Hivyo basi serikali itabidi ishawishi Chama na jumuiya kununua viwanja au shule zake. Vikao vingi vinafanyika vya kutathimini mali za chama na hawapo tayari kupoteza source income yao eti kisa wananchi hamliziki na ubora wa uwanja wao.

Nguvu na makelele mengi zipelekwe kwa katibu wa umoja wa wazazi wa mkoa husika,kwani pesa nyingi ya kiingilio inabaki huko na makao makuu inaenda chache tu. Ubovu wa kiwanja cha mpira au shule ni udhaifu wa katibu wa umoja wa wazazi mkoa na wilaya, Ahsante ndugu.

Nb: Nazungumzia viwanja vilivyo chini ya umoja wa wazaza na jumuiya zingine.
 
Kwanza pole kwa kukosa usingizi, pili pole kwa kilichokukosesha usingizi,tatu pole kwa uwanja uliouona na hadi kuja hapa kutoa maoni.
Viwanja hivi wakati vinajengwa vilikuwa vinajengwa chini ya umoja wa wazazi Tanzania ambayo ni jumuiya hai cha CCM...
Hao umoja wa wazazi ndio waliokuwa wakitoa fedha?
 
Hao umoja wa wazazi ndio waliokuwa wakitoa fedha?
Effect ya serikali kuchukua uwanja ni kubwa kwani hii itahalilisha au kutoa njia ya mali zote za chama zije serikalini ikiwemo shule,viwanja vya makazi,nyumba za kupangisha,vyuo n.k narudia tena hili halitawezekana hata upinzani ukiingia madarakani, najuwa hautanielewa ila njia pekee ya kuchukua serikali ni kuvinunua kwa hiyari ya chama na jumuiya yenyewe.
 
Kwanza pole kwa kukosa usingizi, pili pole kwa kilichokukosesha usingizi,tatu pole kwa uwanja uliouona na hadi kuja hapa kutoa maoni.
Viwanja hivi wakati vinajengwa vilikuwa vinajengwa chini ya umoja wa wazazi Tanzania ambayo ni jumuiya hai cha CCM...
Na wewe hapa unajiona bonge la mshauri? Mkuu wa mkoa ndo alikuwa katibu wa Umoja wa Wazazi? Viwanja vyote vimesimamiwa ujenzi na maRC Kwa nguvu huku Wananchi bila kujali ni wanaccm au la wakishurutishwa kutoa nguvu na Mali zào.
 
Naunga mkono hoja.

Tulichangia ujenzi wa uwanja wa kumbukizi ya George. (almaarufu Memorial) kipindi RC akiwa Mh. Mohammed Babu. Nashangaa Sasa hivi ule uwanja wanauzia mitumba umekuwa soko.

Inasikitisha sana Kwa kweli.
 
Wananchi walichangia nguvu tu ila kuna watu walitoa mpunga wao wa maana kwa mgongo wa chama ili kufanikisha hilo, sikatai wananchi walichangia kama 10% ya ujenzi wa uwanja ila usiaminishe viwanja vilijengwa na wananchi.
 
Naunga mkono hoja.

Tulichangia ujenzi wa uwanja wa kumbukizi ya George. (almaarufu Memorial) kipindi RC akiwa Mh. Mohammed Babu. Nashangaa Sasa hivi ule uwanja wanauzia mitumba umekuwa soko.

Inasikitisha sana Kwa kweli.
Kwani vilivyomo tu ni vingi kuliko hata uwezo wa uendeshaji wa viwanja hivyo. Ccm inanufaika zaidi na uwanja huo hata kuliko maji maji stadium kwani upo tu.
 
Ujenzi huu ulitokana na michango ya wananchi wote bila kujali itikadi au kama ni mwanachama wa CCM au la,kwani kulikuwa na chama kimoja tu.

Na wanaochangia harusi nao wapewe mbususu ya bi harusi kwa kuwa bwana harusi hakugharamia peke yake ni michango ya family and friends.
 
Kwanza vingi ya hivi viwanja vilipaswa viwe vya ‘public’ kwani vilijengwa kwa nguvu zetu wananchi na baadaye vikaja kupirea na majizi - CCM!
 
Kwanza pole kwa kukosa usingizi, pili pole kwa kilichokukosesha usingizi,tatu pole kwa uwanja uliouona na hadi kuja hapa kutoa maoni.
Viwanja hivi wakati vinajengwa vilikuwa vinajengwa chini ya umoja wa wazazi Tanzania ambayo ni jumuiya hai cha CCM...
Hapa umedanganya kabisa.... Viwanja vilijengwa kwa nguvu za wananchi.. Wasimamizi wakiwa Wakuu wa Mikoa.

Mfano: Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, ulijengwa kwa nguvu ya Wananchi, chini ya usimamizi shupavu wa RC wa wakati huo Tumainiel Kiwelu.

Usilete ngojera zako hapa.
 
unahamisha pesa mfuko wa shati na kuiweka mfuko wa suruali!
 
Nchi yenyewe ipo chini ya chama na hatuna mpango wa kuirudisha kwa wananchi🐒
 
Hapo ndipo mnapojidanganya mchana kweupe, ccm kama ccm hawajajenga uwanja wowote katika nchi hii na hili liko wazi, anayepinga anafanya hivyo kwa kiburi chake tu cha kipumbavu.

Wakati hivi viwanja vinajengwa, sisi wengine tulikuwa ni watu wa kujitambua kabisa na ilikuwa ni shughuli ya ujenzi wa taifa sawa na shughuli nyingine yoyote sawa na ilivyokuwa kwa ujenzi wa shule, zahanati au barabara na ilihusisha wananchi wote kipindi hicho cha chama kimoja.

Wakati chama cha Kanu kinatawala nchini Kenya kilijimilikisha ukumbi mkubwa wa Kenyatta International Conference Centre (KICC) kwa miaka mingi sana lakini walipobanduliwa madarakani mwaka 2002 walifurushwa kwenye hilo jengo la ghorofa 28 na jitihada zao za kupinga mahakamani ziligonga mwamba.

Kwa sasa ccm wanaweza kutamba na hizo properties kwa kipindi hiki ambapo bado wapo madarakani lakini muda unakuja ambapo hawataruhusiwa hata kusogelea hivyo viwanja pamoja na majengo mengine.

Kama ccm wanadai hivyo viwanja basi kwa nini wasidai shule, zahanati, hospitali na barabara zote zilizojengwa wakati wa chama kimoja kwa nini iwe viwanja na majengo tu....???

Ni matumaini yangu kwamba hata kama mimi nitakuwa sipo duniani lakini andiko langu hili litakuwepo kama ushahidi kwamba tuliwahi kulisemea hili.
 
Back
Top Bottom