Nadhani na mimi nitapata

Harvest

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
55
Reaction score
31
Nimeona wengi wakitafuta wapenzi na mimi upweke umenichosha.Mwanamke yoyote anaehitaji mume nipo hapa.Umri wangu 29.Sijali umri,dini wala elimu.Kazi yangu ni mbeba mizigo,natumia mkokoteni.Kama utaona sikufai pita usikwazike.Nina mapenzi ya kweli,kama unataka mume wa kweli ni pm tafadhali.
 
Ndugu yangu tatizo litalokukwamisha ni profession yako.. Hapo warembo wengi wataingia mitini. Kie kie kie


Sent via EyePhone
 
Safi sana mkuu na utawapata wengi tu hapa mpaka mwenyewe utachoka.
 
Mkokoteni,bora ingekuwa Guta..
 

Yaani niliposoma tu hili tangazo lako, moyo wangu woteee umekufa juu yako! nimekuzimikia jumla, nahisi una mapenzi ya kweli na unajiamini. Tatizo katika karne hii ya digital tutaishije bila king'amuzi, gari, nyumba, elimu dunia, loooooo niko njia panda.
 
ukipata matatizo kwenye uhusiano wa ndoa unalaumu wanawake wa siku hizi unadhani njia uliyotumia ni sahihi kutafuta mchumba
 

Hivyo vnatafutwa tu!
 
Tehe!tehe! Alifaninikisha Profesa Jay tu! Kwa Zali la mentari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…