Nadhani ni Wakati wa Kagere kustaafu Soka

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Wapo wachezaji wanaozeeka na mpira wao mguuni, kwa mfano Zidane. Lakini wapo ambao mpira hupotea kulingana na umri . .

Kagere enzi zake alikuwa mtu hatari sana , anakufunga katika impossible angles. Kwa Sasa umri umekuwa ni kikwazo kwake ... Hivyo anatakiwa ku staafu kiheshima.

Kqgere wa sasa amekuwa ni mzururaji , anadonoa donoa kama kuku wa Kienyeji na hana madhara kwenye pitch. Kwa Mfano leo , amekosa magoli ya wazi , kwenye mechi za kimataifa... hii kitu haitakiwi.

Nadhan uongozi wa SSC .. ifike pahala waachane nae na waangalie mtu ambaye atafaa kwa replacement au wafanye usajili

Mpira ni biashara, kukosa magoli unnecessarily ni sawa na kukataa wateja kwenye biashara, ni HASARA.

Kagere apumsishwe..:.. wakati wake umefika
 
Msimo ujao simba tusajili washambuliaji wawili wa kimataifa wenye viwango vya hali ya juu kabisa na ikiwezekana na mmoja wa ndani na namba 5 mmoja tosha kabisa ni wakati wa kuwapa mkono wa heri kagere na Mugalu
 
Baada ya Bocco kupata mganga mpya sasa tuhamie Kwa Kagere,akiperform vizur tuende Kwa Mugalu....Pengine tukiwasema sema hivi wataimpruv.
 
Wapo wachezaji wanaozeeka na mpira wao mguuni, kwa mfano Zidane. Lakini wapo ambao mpira hupotea kulingana na umri...
Twendelee kumuingisha MO kwa kununua MO Xtra, Mo protector
 
Usituletee mambo yako ya Utopolo hapa. Simba haikuhusu tena koma kabisa!
 
Msimo ujao simba tusajili washambuliaji wawili wa kimataifa wenye viwango vya hali ya juu kabisa na ikiwezekana na mmoja wa ndani na namba 5 mmoja tosha kabisa ni wakati wa kuwapa mkono wa heri kagere na Mugalu

Umeenda vyema Kaka
 
Sasa mmehamia kwa Kagere??, Acheni wachezaji wacheze mpira hakuna binadam ambaye anaweza kuwa kwenye kilele cha mafanikio wakati wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…