Nadhani Simba waache ujinga wa "sijui pira biriani"

Nadhani Simba waache ujinga wa "sijui pira biriani"

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Mpira ni magoli.
Hii dhana ya kucheza entertaining football naona ni ya kijinga sana.Maana inategemea vitu vingi sana ili ifanikiwe. Mfano mechi ya jana na Prisons. Prisons wamecheza Mpira wa nguvu na vurugu sana.Uwanja wenyewe hauruhusu hizo pasi za rula.Kasi ya wachezaji wa Simba siyo kubwa.Upangaji wa timu na game plan mbovu.Huwezi kupata matokeo kwa jinsi hiyo.

Simba wawekeze kwenye kupata ushindi na waachane na maneno ya Haji. Kuna baadhi ya watangazaji wanasifia eti "soft touch" huu ni upuuzi mkubwa. Mpira wenyewe ni wa kiume hivyo uwekezaji wa nguvu lazima uende sambamba na akili na kipaji.

Kutokana na hii dhana na falsafa ya pira biriani imesababisha wachezaji kama Miqueuson na Morrison waache aina ya mchezo wao uliokuwa unaleta hatari sana kwa timu pinzani.Haya mambo ya chenga twawala ni ya kizamani sana
 
Simba walikua mbumbumbu tangu zamani Ila Haji Manara amewafanya wamekua zaidi ya ma mbumbumbu. Wamecheza mechi ya kirafiki na mlandege ya Zanzibar wakashinda Goli tatu Basi Wana aminishwa wao Wana kiwango Cha juu sana katika soka.
 
Maneno ya kishabiki tu hayo ni ya kawaida kwenye michezo, hata timu nyingine zinaweza kutafuta naneno yao ya kuwahamasisha,sijaona shida yoyote ile,kupoteza game moja sio sababu ya kutoendelea kufanya vizuri tena
 
Hujui mpira wewe...Kufungwa kupo tu...hata ucheze mpira wa vurugu kama walivyofanya Prison. Jiulize Prison hushinda mechi ngapi kwa msimu na mpira wao unaoshauri Simba icheze?

Eti "wamefungwa kisa mpira biliani" yaani hujui hata kwanini Simba inaitwa Lunyasi unataka kujifanya shabiki? Kila timu inafalsafa yake na husajili kocha na wachezaji kutokana na falsafa yake.

Mpira ndo ulivyo kama hutaki kufungwa kacheze Video game ili ucheze kwa mfumo wako usitupangie.
 
Hujui mpira wewe...Kufungwa kupo tu...hata ucheze mpira wa vurugu kama walivyofanya Prison...Jiulize Prison hushinda mechi ngapi kwa msimu na mpira wao unaoshauri Simba icheze?
Eti "wamefungwa kisa mpira biliani" yaani hujui hata kwanini Simba inaitwa Lunyasi unataka kujifanya shabiki? Kila timu inafalsafa yake na husajili kocha na wachezaji kutokana na falsafa yake.
Mpira ndo ulivyo kama hutaki kufungwa kacheze Video game ili ucheze kwa mfumo wako usitupangie.
Ume-Comment kwa hasira ya hali ya juu sana,tulia mkuu,Simba huwa ikishinda ooh umeona lile pira wakifungwa ooh opponent wenu walikuwa wanacheza mpira wa vurugu/kubutua,tulieni na msijiaminishe saaaana kwamba mnajua mpira mazee,always mpira una matokeo mabaya sana,hii dhana ya kwamba mnakikosi kipana inatakiwa ibakie kama stor tu and not by confidence.
 
Soma vizuri kilichoandikwa uelewe ndo U comment...siyo unakurupuka tu au una hangover?
 
Mpira ni magoli.
Hii dhana ya kucheza entertaining football naona ni ya kijinga sana.Maana inategemea vitu vingi sana ili ifanikiwe.
Mfano mechi ya jana na Prisons.
Prisons wamecheza Mpira wa nguvu na vurugu sana.Uwanja wenyewe hauruhusu hizo pasi za rula.Kasi ya wachezaji wa Simba siyo kubwa.Upangaji wa timu na game plan mbovu.Huwezi kupata matokeo kwa jinsi hiyo.

Simba wawekeze kwenye kupata ushindi na waachane na maneno ya Haji.
Kuna baadhi ya watangazaji wanasifia eti "soft touch" huu ni upuuzi mkubwa.
Mpira wenyewe ni wa kiume hivyo uwekezaji wa nguvu lazima uende sambamba na akili na kipaji.

Kutokana na hii dhana na falsafa ya pira biriani imesababisha wachezaji kama Miqueuson na Morrison waache aina ya mchezo wao uliokuwa unaleta hatari sana kwa timu pinzani.Haya mambo ya chenga twawala ni ya kizamani sana
We jamaa sio mwanasoka..acha kupanic bila sababu mkuu...last game ya vpl mlishinda 4-0 na mkasifia pira birian, wala hatukusikia swala la upangaji mbovu wa kikosi...Leo mmefungwa unakuja na pointless...Mkishinda bila biriani mnalalamika....kufungwa ni kawaida mkuu...Basi hakuna maana ya ligi ikiwa mnataka kushinda game zote..nyie hata mkisuluhu mnaanza lawama kibaooo...

NB: msirudie kupeleka biriani kwa wajelajela.
 
Ume-Comment kwa hasira ya hali ya juu sana,tulia mkuu,Simba huwa ikishinda ooh umeona lile pira wakifungwa ooh opponent wenu walikuwa wanacheza mpira wa vurugu/kubutua,tulieni na msijiaminishe saaaana kwamba mnajua mpira mazee,always mpira una matokeo mabaya sana,hii dhana ya kwamba mnakikosi kipana inatakiwa ibakie kama stor tu and not by confidence.
Umehama kwenye pira biriani umeingia kwenye kikosi kipana..Ngoja nikwambie kitu mkuu, kufungwa na prison sio ishu sana sababu hakuna timu duniani ambayo haifungwagi..Moyoni mwako mwenyewe unajua na unakiri kwamba Simba ni zaidi mara kumi ya timu yako unayoishangilia..
 
Simba kufungwa na Prison sio kitu cha ajabu sana kwani hakuna timu ambayo haifungwi duniani. Lakini kuna haja ya uongozi kuangalia kati ya Manula na kocha wa magolikipa nani mbovu kati yao. Hii ya Manula kukosa "timing" ya mipira ya kona na krosi kila wakati imekuwa inaigharimu Simba mara kwa mara. Hili lisipoangaliwa kwa umakini mapema basi wajiandae kabisa na dhahama kwenye ligi ya mabingwa Afrika naona zile tano tano safari hii zitaongezeka zaidi.

Na benchi la ufundi nalo liwe linabadili mbinu za mchezo. Timu ipo mkoani huko uwanja haulingani na wa Mkapa halafu mnataka mcheze mpira biriani badala ya kutafuta ushindi kwa njia yoyote ile. Kama benchi la ufundi lingekuwa makini ndani ya dakika 15 za mwanzo lingebadili mbinu kwani ndani ya dakika hizo Simba ilifika kwa shida sana tena mara chache kwenye lango la Prison. Hiyo ilitosha kabisa kulishtua benchi la ufundi la Simba kuwa pale katikati hakuna njia ya kupitisha mipira Prison wamebana lakini wapi lilikuwa kama sikio la kufa halisikii dawa. Kwa mechi ya jana Simba ilipaswa icheze mipira mirefu kuelekea kwenye lango la Prison ili kuwalazamisha wafanye makosa kwenye safu yao ulinzi na wao wayatumie hayo makosa. Lakini wapi timu ilicheza na kumaliza mchezo kwa mbinu zile zile za pasi fupi fupi mwanzo mpaka mpira unaisha wakati huo wanakuwa wanawapa Prison nafasi ya kujipanga nyuma na mbaya zaidi hata zilipobaki dakika 15 za lala salama bado Simba ilikuwa inacheza tu "square pass" a.k.a pira biriani nyuma badala ya kupeleka mipira haraka mbele kabla Prison hawajajipanga vizuri.
 
Kuna jamaa angu kanitumia hii.
255767086767_status_634a45be3fb4403ab7bf05994ffd2567.jpg
 
Simba kuna tatizo hilo matatizo hatuyaoni kwa sababu tumezoea kupata ushindi .
Kwa kifupi kocha wetu anabebwa na wachezaji hana plan b, anachezesha timu kwa kukariri labda atueleze kama anapangiwa kikosi kwani mchezaji kama Dilunga kiwango kimeshuka lakini mara nyingi anaanza.
Mchezaji kama Kahata anakaa benchi haya mambo yamesababisha kuacha wachezaji wazuri kama Shibob , Kanda kwa kuwasugulisha benchi na leo hii kama sio mkude kuumia tusingejua uwezo wa Fraga.
Timu imeingia uwekezaji lakuni inashindwa kuajili kocha wa maana wa makipa kina Mwameja wapo tena wana vyeti lakini unakaa na kocha asiye na vyeti huu ni udhaifu mkubwa.
Tukitolewa mapema hatutaki kusikia vijisababu Zambia walipuuzia matokeo yake waliyaona.
 
Hujui mpira wewe...Kufungwa kupo tu...hata ucheze mpira wa vurugu kama walivyofanya Prison. Jiulize Prison hushinda mechi ngapi kwa msimu na mpira wao unaoshauri Simba icheze?

Eti "wamefungwa kisa mpira biliani" yaani hujui hata kwanini Simba inaitwa Lunyasi unataka kujifanya shabiki? Kila timu inafalsafa yake na husajili kocha na wachezaji kutokana na falsafa yake.

Mpira ndo ulivyo kama hutaki kufungwa kacheze Video game ili ucheze kwa mfumo wako usitupangie.
Kama hajakuelewa apa basi tena Mkuu.
 
Back
Top Bottom