Nadhani

Nadhani

Kichankuli

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2008
Posts
887
Reaction score
190
Neno Nafikiri humaanisha kufanya uchambuzi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa jambo fulani kwa kutumia ubongo. waingereza hutumia "I think"

Neno Nahisi humaanisha utambuzi wa jambo au hali fulani kwa kutumia viungo vya au/na maumbile ya mwili. Waingereza hutumia "I feel"

Lakini neno Nadhani japokuwa nalitumiaga lakini sijajuwa linatumia nyezo ipi katika mwili wa binadamu katika utendaji. Wadau wa lugha mnipambanulie tafadhal
 
Tofauti kati ya fikiri na dhani:
Kufikiri ni matumizi ya akili; kudhani inahusu pia matumizi ya akili lakini kiwango cha uhakika ni kidogo; ni kufikiri bila kuwa na uhakika (tazama [ame="http://sw.wikipedia.org/wiki/KKS"]KSS[/ame]); inaelekea zaidi upande wa "kuhisi".

Wenzangu wanaonaje?
 
Je kwa yule mwenye kusema... "Nahisi njaa, Nasikia njaa au Naona Njaa" Neno lipi ni sahii hapa.

Nimeuliza hivyo kwa sababu mara nyingi nawasikia watumiaji wa lugha ya kiswahili wakiyatumia maneno hayo niliyo yakoza hapo juu.
 
Naona kusikia njaa na kuona njaa zote mbili sawa na Kiswahili sanifu. "Kuhisi njaa" - sidhani ya kwamba ni sanifu.
 
Back
Top Bottom