Neno Nafikiri humaanisha kufanya uchambuzi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa jambo fulani kwa kutumia ubongo. waingereza hutumia "I think"
Neno Nahisi humaanisha utambuzi wa jambo au hali fulani kwa kutumia viungo vya au/na maumbile ya mwili. Waingereza hutumia "I feel"
Lakini neno Nadhani japokuwa nalitumiaga lakini sijajuwa linatumia nyezo ipi katika mwili wa binadamu katika utendaji. Wadau wa lugha mnipambanulie tafadhal
Tofauti kati ya fikiri na dhani:
Kufikiri ni matumizi ya akili; kudhani inahusu pia matumizi ya akili lakini kiwango cha uhakika ni kidogo; ni kufikiri bila kuwa na uhakika (tazama [ame="http://sw.wikipedia.org/wiki/KKS"]KSS[/ame]); inaelekea zaidi upande wa "kuhisi".