Nadharia Kuhusu Kulogwa (Kulishwa) na Ramli

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Habari za sahizi wakuu!

Kuna Nadharia (Japo sina uhakika) kwamba mtu akilogwa yaani kulishwa atabaki kuumwa tumbo tu lakini Hospitali atakuwa Hatibiki..Je mtu wa dizaini hii anasaidikajee?

Pia kuna Nadharia ingine kwamba unaeza enda kwa Mpiga Ramli akakuambia kama wewe umelogwa au umelishwa au akakuambia pia na wachawi wako au pia mwanamke/mwanaume anayekufaa (mfano awe mweusi/mweupe)...Je kuna ukweli wowote pia Hapa? au ni watu wanapiga tu Pesa!
 
Hamna ukweli wowote hapo kupiga hela tuu,na kuchonganisha watu mkuu.
 
Kuna rafiki angu mmoja hivi alikuwa asimamishi mashine, kwenda kwa mganga akaambiawa Aunt zako ndio wamefanya hivyo, Jamaa akatoka akabeba panga mpaka kwa shangani zake akawatisha kuwaua na akawapigia mtwara kuwa kufikia siku tatunataka mjeshi wangu apige saluti, Mbona siku ya pili alirudi hewani.
Ndipo nilianza kuamini hivi vitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…