nadharia ya uhalifu

nadharia ya uhalifu

illegal migrant

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
1,277
Reaction score
1,121
leo nataka tuingie darasani kidogo ila ntalifupisha somo, nadharia ya uhalifu ni sababu zinazofanya watu aina Fulani kupendelea kufanya makosa ya aina Fulani mfano vijana wa miaka ishirini kupendelea kuvuta bangi, ama kabila Fulani kupendelea kufanya makosa Fulani, kwa askari aliyesoma criminology unapopeleka malalamiko pale kituoni atakwambia huyo aliyekufanyia kosa hilo lazima atakuwa mtu wa aina Fulani yaani kikabila umri nk .

hapa tunapata dhana kuwa wahalifu wote wanasukumwa na vitu Fulani ili watende uhalifu, wengine dhiki, wengine umri wa ukuaji, na nyingi zingine leo nataka nizungumzie aina ya uhalifu yenye athari ya moja kwa moja kwenye taifa letu mfano tunapozungumzia ubadhirifu kwenye mashirika/ mataasisi naomba ieleweke kwamba muhusika kabla ya kutenda kosa anakuwa na akili zake timamu, mfano mkurugenzi wa halmashauri anapoamua kuiba million mia mbili za mradi, pale anakuwa ame wa consult wanasheria tayari manake anakuwa amejipanga matokeo yake CAG akienda kufanya mahesabu yake na kukuta kuna mapungufu watafikia uamuzi wa kumfukuza/ kumsimamisha kazi kufukuzwa kazi kwa mkurugenzi huyu kutakuwa neema kwake kwani katika mahesabu aliyopiga alijua ya kwamba hapa nikifanya kazi mpaka kustaafu sitaweza kupata hiyo mil 200.

kwa hiyo huyu jamaa bado utakuwa hujamkomoa kwa upande mwingine huyu jamaa akifunguliwa mashitaka, kwa sababu alikuwa amejipanga na wanasheria wake uwezekano wa kushinda kesi kwa upande wake unakuwa mkubwa na akishinda kesi anafungua mashitaka ya kuchafuliwa na itabidi alipwe kipindi ambacho alikuwa ameshimamishwa kazi hivi ndivyo hela za serikali yetu zinavyopotea kuna kitu kinaitwa loss prevention hapa ndio serikali ingetilia mkazo kwa hiyo kuna haja ya kuwa na wataalamu wa masuala ya usalama na mali zao kwani kwa sasa elimu ya usalama wa raia ni ya kidarasani zaidi tusisubiri mpaka mtu akosee ndio tumfungulie mashitaka bali tuzibe ile mianya ya ushawishi nadhani kama umewahi kufanya kazi kwenye mashiriki ya wafadhili (donor funded projects) utanielewa nacho sema wana mfumo mzuri wa udhibiti kama watu wanaiba basi wanaiba vilaki laki tu.
 
Back
Top Bottom