Naelekea kuzama penzini

kikaniki

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
508
Reaction score
968
Wadau, habari zenu.

Ni mtumishi serikalini. Ofisini kwetu kuna mrembo mmoja (nikisema mrembo, ninamaanisha mrembo). Huyu dada kwa takribani miaka 4 tuliyohudumu nae hapa kazini, amekuwa akipa heshima ya kaka na mimi nikimuona kama dada yangu mdogo.

Sasa kisanga kikaanza, siku moja tukiwa kikaoni, ndani ya kikao nikawa nachati na mtu mwingine. Huyo dada akaniandikia katika kikaratasi, "usichati. Napata wivu". Na imekuwa ni kama ada, akisikia tu simu yangu inaita, lazima aje aangalie ni nani anapiga na ni nani naongea nae. Lakini pia, weekend amekuwa akiniomba kama nina nafasi, basi nimtoe outing.

Nina mke na yeye ni mke wa mtu. Nafanyaje?
 
kwani mkeo anasemaje?
 
But how?
 
Sema unaonekana ukiiba mbona unalamba na mwiko kabisa.....
Wakati masharti ukiiba mbona hutakiwi kuiiba mwiko.

So far, wizi mwema
 
Operesheni kataa ndoa inapata nguvu sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…