Naenda jimboni... Nitawamiss sana

Mzee wa docebit... yaani kama nakuona ulivyomaind huyu dude!!! Inawezekana kabisa anaandika ka-study au assignment ya sociaology huko alipo na hapa ndio venyu ya kupata respondents badala ya questionnaires

Mpotezee aisee

Amani Omnia

Pamoja sana.....VOS OMNIA!
 
Mkuu,

Nakutakia mafanikio mema huko wilayani. Tumesema sana na inabidi wengine kujiingiza huko na kujaribu kufanya yale yaliyowashinda wengi.

Kama unataka baadhi ya TIPS tuwasiliane kwa PM japo sina uzoefu mkubwa ingawaje miezi mitano ya kuwa kwenye firing line kwa vyovyote kuna vitu nimejifunza.

I am for change na yeyote anayeamini katika mabadiliko ya kweli bila kujali yuko kambi gani, mimi nitampa japo moral support. Wengine mabingwa wa kusema lakini vitendo sifuri. Matendo huvuma zaidi ya maneno matupu.

Safari njema na mafanikio mema.
 

Hapo ndio napata shaka. Malengo yako ni thabiti kuwa unataka kuwa mbunge, na unachopigania nadhani kinaeleweka. Katika hiyo equation sioni kama umeweka agenda ya maendeleo ya mtanzania. Hata hivyo kila la kheri katika malengo yako. I may be wrong though...
 

Sidhani kama kuamua kugombea ni ushujaa kama mnavyotaka tuelewe. Na si lazima wote wawe front line kwenye battle, wengine tunaweza kuwa kubaki kama critics ili msione mawazo yenu ni gospel truth.
Ninapata shaka na mabadiliko mnayotaka kuyaleta, nilidhani tunaweza kubadili hii monopoly ya power katika nchi, kwani ndio inaonekana kuwasahaulisha watu wengine na kujifanya majimbo na uongozi ni kwao tu. The fact that wote mnang'ang'ania kugombea kupitia CCM kwa sababu ni chama ambacho kina himaya kongwe inanipa shaka kuwa either hamna confidence or you are simply cowards and selfish.
Mnachoita mabadiliko kwenu ni ninyi kuingia madarakani, kuendeleza utamaduni ule ule wa CCM, badala ya wale waliopo sasa.
Kama mnajiamini kuwa mnakubalika, mnaweza kurise kwenye chama chochote cha siasa, badala ya kupoteza muda wa miezi mingi kulumbana na watu waliohodhi madaraka, nani alikuambia kuwa ubunge ni lazima upitie CCM?

Nazidi kupata shaka sana kuhusu fikra zetu za mabadiliko na future ya nchi yetu.

/sorry...
 



Kila la kheri mheshimiwa mtarajiwa,ila tu la msingi huko jimboni usiwe unaenda kutoa pesa takrima ilishazuiwa,kuhusu ughaibuni angalia usije ukaslimu na kuuza jimbo lako kwa manyangau!!!!!!!!!!!!!
 
Umeogopa nini kuchukua fomu ya urais? au vitisho vya yule nanii? na akisema atakayempinga mbunge wa hilo jimbo lako naye atananii je utajitoa kama shibunanii?
 
Nenda mgombea, huenda tutakutana huko, kwani nami niko njiani. Wakati ni huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…