Occupy
Member
- Jul 4, 2022
- 9
- 13
Habari wakuu,
Watu hatuna STATUS sawa kwenye jamii ndio maana nimekuja kuomba msaada.
Mimi ni mjasiriamali baada ya kuhitimu chuo mwaka jana nilikuwa nimejibana nikasevu pesa kidogo nikanunua Mashine za kukoboa na kusaga Mahindi (Mota na vinu viwili) ni miezi minne sasa tangu ianze kufanya kazi.
Chanzo cha kuja kuomba msaada ni baada ya MITA kuungua ikabidi nifunge biashara nikaanza kufuatilia msaada TANESCO waje kunifungia MITA mpya, hapa shida ilipoanzia umepita mwezi sasa kila siku napewa ahadi.
Kinachoumiza kichwa hii biashara ilihitaji mtaji mkubwa ambao sikuwa nao ilibidi nikope pesa nyingine kuongezea, na ninategemea kulipa kupitia mradi huu huu kwasababu nilibahatisha eneo lina wateja sana na wa uhakika.
Napata stress sana nitaishije ukizingatia nilishashuhudia watu kadhaa waliowahii kukaa hadi miezi 3 wakisubiri kubadilishiwa mita iliyoungua hapo ndo nachoka zaidi, naona dalili za kupoteza vitu vyangu kisa madeni.
Naomba kwa mwenye connection nzuri na TANESCO anisaidie nipewe huduma kwa haraka nimekwama.
Nipo Tabora
Natanguliza shukrani.