Kiagoh92
Senior Member
- Feb 23, 2018
- 101
- 56
NAENDA KUOA PEMBA.
Naenda kuoa Pemba, msichana wa Kojani
Yule anaejipamba, kwa mitandio kitwani
Aongea kwa kutamba, na lafudhi ya kipwani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Kojani nikimkosa, natafuta Mkoani
Niweze peleka posa, ili nipate mwandani
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nikaoe Wete, nikikosa Mkoani
Nende nimvishe pete, yule ninomtamani
Tena niwazidi kete, hao wangu washindani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nende Shengejuu, tena kule ndani ndani
Nipate mwenye nafuu, aniliwaze moyoni
Kwa maji ya karafuu, anikande maungoni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Naulizia Kengeja, naomba nipelekeni
Kwa wanouza vileja, tosi halua ubani
Namuhitaji mmoja, sisikii na sioni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Wakazi wa Chakechake, hasa wa hapo mjini
Msije nipiga teke, nikafia baharini
Msiniache mpweke, niozesheni jamani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Ndugu zangu wa Kianga, naomba nipokeeni
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni
Kama nyumba nitajenga, hata pale Mnarani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nisogee Wingwi, sababu wanithamini
Najua pale sipingwi, hata kama masikini
Sitozamishiwa Nungwi, nikiwa na hali duni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Sebu pasahau Konde, napapenda kama nini
Taenda hata kwa mbinde, kwa uwezo wa Manani
Nahitaji anikande, nitaporudi kazini
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Hapa kituo niweke, kalamu niweke ttini
Wapi posa nipeleke, mawazo tele kitwani
Nioe nifurahike, raha ya ndoa ndoani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Naenda kuoa Pemba, msichana wa Kojani
Yule anaejipamba, kwa mitandio kitwani
Aongea kwa kutamba, na lafudhi ya kipwani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Kojani nikimkosa, natafuta Mkoani
Niweze peleka posa, ili nipate mwandani
Naenda haraka hasa, nisichelewe njiani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nikaoe Wete, nikikosa Mkoani
Nende nimvishe pete, yule ninomtamani
Tena niwazidi kete, hao wangu washindani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nende Shengejuu, tena kule ndani ndani
Nipate mwenye nafuu, aniliwaze moyoni
Kwa maji ya karafuu, anikande maungoni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Naulizia Kengeja, naomba nipelekeni
Kwa wanouza vileja, tosi halua ubani
Namuhitaji mmoja, sisikii na sioni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Wakazi wa Chakechake, hasa wa hapo mjini
Msije nipiga teke, nikafia baharini
Msiniache mpweke, niozesheni jamani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Ndugu zangu wa Kianga, naomba nipokeeni
Nakuja kutia nanga, nimsake wa moyoni
Kama nyumba nitajenga, hata pale Mnarani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Au nisogee Wingwi, sababu wanithamini
Najua pale sipingwi, hata kama masikini
Sitozamishiwa Nungwi, nikiwa na hali duni
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Sebu pasahau Konde, napapenda kama nini
Taenda hata kwa mbinde, kwa uwezo wa Manani
Nahitaji anikande, nitaporudi kazini
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.
Hapa kituo niweke, kalamu niweke ttini
Wapi posa nipeleke, mawazo tele kitwani
Nioe nifurahike, raha ya ndoa ndoani
Naenda kuoa Pemba, alo na njema tabia.