Nafanya biashara ya Miamala. Naombeni ushauri wenu

mfuga kuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2014
Posts
824
Reaction score
650
Wanabodi biashara hii itaniua kwa pressure, tangia nimeianza sijawahi pata pesa zaidi napata hasara tu. Mara ya kwanza ni miezi mitatu iliyopita nimepata short ya 200,000/= leo nimechek nimekuta short ya 150,000/=

Hebu wajuzi wa mambo nishaurini, namna ya udhibiti.
 

Short inakuwaje kwani kile kitabu cha miamala unacho. ujue ulicho nacho au kinachotoka
 
Zinakua zinaenda wapi kwani? Ina maana Kila siku jioni hufungi hesabu?
Huwa sifungi huwa naangalia kamishen ya kila mwezi na kuwaelekeza vijana wanote hiyo ktk kitabu. mfano.
1. September kamishen 20,000/=
2. October 21,000/=
3. Novemba 21,500/=

kisha najumlisha na lile salio langu nililowekeza najua kiasi kinachoongezeka
 
Inawezekana ndio anaanza usimbeze, kadri anavyokua na wateja wataongezeka.
Ni kweli sina muda mrefu nimeanza na line 3 tu! lkn bado nahitaji kujua namna ya udhibiti wa ile fedha ili hata nikiongeza mtaji isinipe shida.
 
biashara ya mpesa ni pasua kichwa saivi funga haraka. serikali imeweka makato mengi sana mawakala wanapata ela ndogo mno ata ukileta lipa namba bado hela ni ndogo. funga hama iyo biashara kabla hujatapeliwa na kuua kabisa mtaji
Duh!
 
Tafuta LIPA NAMBA wanaotoa wote tumia lipa namba. Mfano mtu anataka kutoa Laki moja, analipa 102,000 unampa 100,000 Kamili. Miamala ya kuweka tu ndio tumia Till. Tofauti na hapo ukikomaa kawaida hata kodi utakosa, mtaji wote utaisha unajiona
Ahsante bila shaka hii itakuwa njia bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…