Nafanya biashara ya Miamala. Naombeni ushauri wenu


Njoo pitia lita tano ya mafuta ya alizeti hapa misuna
 
Hiyo biashara waliofaidi Ni wale walifungua zamani,na kwa huo mtaji wako ,hakuna kitu Apo,Bora ungekua na mtaji mkubwa,na siku hizi laini moja tu ,mwanzo ilikua Kuna laini ya float,ata Kama haupo dukani wewe kila kinachofanyika laini hiyo ya pili unabaki nayo wewe,unakua unajua
 
Au sio!?[emoji2]
 
Ukiachana tu na kutokufunga hesabu hiyo commision tu ni ndogo sana. Hapo hakuna biashara

Nimeanza biashara ya miamala mwezi wa 9 na commission ya kwanza kwa mitandao yote mi4 (Tigo, Voda, halotel, na Airtel) ilikua 21 ila mwezi wa 12 nimeingiza commission ya 310,000 kwa mitandao yote mi4.

Usimvunje moyo, MWANZO MGUMU.

#YNWA
 
Niliyembaini ananidokolea nimuondoe au nikae nae chini ili kumjenga na kuendelea kumtumia? mwenye uzoefu na hili wandugu.

Mi dukani kwangu kijana akizingua ni KWAO.
Sinaga masihala na hela.

Mi nina duka la vinywaji, wiki mbili zilizopita nilimkuta kijana anakunywa bia moja store, hapohapo nikafukuza na nilimpa 20,000 kwa huruma asepe nayo, maana ili Baki wiki uishe mwezi.

Usiwe na huruma kwa wasio na huruma na wewe.

#YNWA
 
hyo commision mtaji wake ni tsh ngapi na mzunguko wa wateja upo vipi?
ni centre iliyochangamka au ni sehemu ya kawaida?
Ninatamani kuanza hii biashara naomba kuelekezwa zaidi
 
Funga hesabu daily. Chukua salio la flot jumlisha na salio la cash. Fedha haitakiwi kuzidi au kupungua mpaka mwisho wa mwez utakapotumiwa gawio
 
Mkuu hii shule umetoa hapa ni ya ada kubwa sana ila umetoa bure, ubarikiwe na commision zizidi kuongezeka
 
Nimeanza biashara ya miamala mwezi wa 9 na commission ya kwanza kwa mitandao yote mi4 (Tigo, Voda, halotel, na Airtel) ilikua 21 ila mwezi wa 12 nimeingiza commission ya 310,000 kwa mitandao yote mi4.

Usimvunje moyo, MWANZO MGUMU.

#YNWA

Inategemea na sehemu alipo, mimi December nimepiga 400, 000 kwa tigopesa pekeake. Hapo bado voda, Artel na Halotel. Ubaya wa hizi biashara miezi haifanani
 
Mkuu we ni mfanyabiashara kweli!?
Kwanza hamna biashara inaendeshwa kwa stail hiyo,

Kosa la kwanza
Kuwaamini kupitiliza
Kutofuatilia mwenendo wa biashara
Kuwa mzembe uliyepituliza
Kwa nini uangalie kamishen tu usifuatilie mwenendo wa biashara yako?
Je huyo uliyemgundua analeta mapenzi kwenye hela yako je unajua ni mara ngapi anafanya hivyo?
Kwa nn usimuulize hizo shiti za awali zimetokeaje? Atakuwa anajua mbane

Nina wasi wasi pia hata stationary wanakuibia sana kwa kuwa wamegundua udhaufu wako,
Usipokuwa makini watafungua biashara kama yako pembeni yako na utakuwa umetolewa nje ya reli

Kwa nini unakuwa mzembe hivi?


Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli mmoja nimbaini kamtumia mpenzi wake salio! imeniuma sana lkn sijamuuliza naugulia shingoni.
Hao vijana ulio waajiri ndiyo wanakupiga. Na ukiweka mtaji mkubwa, wazee wa kazi nao watakutembelea (matapeli, vibaka, wezi, na majambazi).

Achilia mbali baadhi ya vibinti, na hata wamama wenye tamaa watakao jipitisha, ili kuifilisi kabisa hiyo ofisi.


NB:- Biashara inataka usimamizi wa karibu. Haitaki umwamini mtu/kijana kwa 100%.
 
Huyu anastahili kuchapwa fimbo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…