Nafanya kazi na nimeajiriwa ila ni ngumu balaa nataka hata kuacha japo sijapata ingine

Ombeni Mbise

Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
40
Reaction score
9
Wadau nimeajiriwa na kusaini mkataba ila kazi ni ngumu sana nataka kukimbia.sijui mnanishaurije coz kuna wengine wamenishauri nisiache coz mtaani ni pagumu xana
 
Skilled au unskilled?
Qualification?
Hz zaweza kuwa sababu ya hayo
 
pole sana , vumilia wakati unafanya bidii ya kutafuta nyingine, kupata kazi ni kazi, na mtaani ni pagumu sio utani.
 
Kiongozi hakunaga kazi nyepesi inategemea hiyo kazi yako umelinganisha na kazi gani mpaka ukaona ya kwako ni ngumu,
kwa ushauri mkuu,we acha hiyo kazi ngumu uone ilivyo kazi ngumu kupata kazi hata ngumu mtaani ukiwa hauna hata hiyo kazi ngumu
.
 
nakushauri usiache....there is no shortcuts mkuu,tena una bahati kupata kazi ngumu maana utakuwa na experience zaidi by working under pressure.kaa hapo chukua maujuzi,jifunze na mambo mengine kutoka department zingine za hapo.at the same time keep applying for similar jobs,na usiache tu kwa sababu unaenda sehemu nyingine kwenye kazi rahisi,zingatia kuongezeka kwa kipato na oportunities zingine utazozipata....tafadhali usikurupuke katika hili.....kila la heri
 
Wadau nimeajiriwa na kusaini mkataba ila kazi ni ngumu sana nataka kukimbia.sijui mnanishaurije coz kuna wengine wamenishauri nisiache coz mtaani ni pagumu xana

Pole sana vumilia tu ndo kutafuta kwenyewe huko kaka mtaani pasikie tu, Alf hii kwenye mabano sio uandishi mkuu (xana)
 
hakuna kazi ngumu kama kupata kazi, jaribu kuwa mvumilivu
 
Karibu mtaani uone hadi inzi wa nyumbani kwenu watakujua kwa kukaa nyumbani.
 
Wadau nimeajiriwa na kusaini mkataba ila kazi ni ngumu sana nataka kukimbia.sijui mnanishaurije coz kuna wengine wamenishauri nisiache coz mtaani ni pagumu xana

acha tu, unaomba ushauri wakati majibu unayo.
 
Kijana hebu tueleze vizuri ni ugumu gani unaokutana nao hapo kazini ili tukusaidie kwa ushauri wenye tija.
 
wadau nimeajiriwa na kusaini mkataba ila kazi ni ngumu sana nataka kukimbia.sijui mnanishaurije coz kuna wengine wamenishauri nisiache coz mtaani ni pagumu xana


hebu vumilia vumilia kwanza
ni kweli mtaani hku kugumu sana
wenzako wanasota sana
 
Jamani siwezi taja shirika gani nafanya watanishtukia, ila sio LOAN OFFICERS kama wengine mnavyodhani. nimepokea ushauri wenu nitaedelea kuwepo kimtindo hadi nipate pengne. Asnteni sana kwa ushauri wenu ila kweli sitaweza watajia kwa sababu ninazodhani zitaniathiri.
 
Usiache kazi kabla haujapata kazi ndugu yangu,mahospital madawa bei ya ghari mtaani pesa hakuna tunalia njaa kali.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…