Nafanya uwekezaji wa Nguruwe

project ya kibabe, hapo uwe na mtaji mtamu siyo magumashi.
mkuu hzo breed unazitambuaje kama mtu siyo mtaalamu. ipi breed nzuri kwa kuvunwa nyama tu (inayojaa nyama haraka)
Mimi nimechanganya but naona Largerwhite, saddleback ni Nzuri sana haijai mafuta,, Duroc inakuwa haraka sana but mafuta ni mengi usipobalance chakula kitakachozuia mafuta ananenepa sana but ni Nzuri tuu
 
Kwavile unafuga kibiashara manake jikite kuwapa lishe ya nyama kuliko mafuta. Njia mojawapo nzuri ni nunua drum moja la morasis. Uwe unakata nyas au maboga na kuwawekea kdogo kidogo. Linakaa sana. Utafaidika sana. Mradi wako mzuri hata mimi kama si kuheshim waisram ningefanya. Na pia kama si kuwaheshim wakristo ningefanya. Mana suala la Yesu kuagiza mapepo waingie kwa nguvu kwa kitoweo cha watu, sijui alimaanisha nini! Je mfugaj alimfidiaje!
 
Vitu vingine vibaya/dhambi unafanya ila kufuga tu nguruwe unaogopa?
 
Hapa mkuu tupe ratio..!nyasi kavu au mbichi..?na kiasi gani cha nyasi vs mollases.
 
Biblia sio kila unachosoma kipo kama kilivo,pengine nguruwe ilimaanisha watu wasio na mwelekeo wowote mzuri wa kiimani. Unawezaje kuhakikisha kuwa ni nguruwe wanyama ilhali Mungu ashatakasa wanyama wote kuwa si najisi (alipomwambia Petro kupitia ndoto kwenye Acts of Apostles)
 
Nakushauri kupeleka machinjioni..!pia fungua bucha zako pamoja na kushika majiko kwenye baadhi ya baa..!usisubiri kufikisha nguruwe 400 ndio uanze kuuza..!inaweza pita swine ukalia..!tengeneza wazazi uwe unauza kwa groups kila baada ya miezi 2-3 unapeleka nguruwe sokoni
 
Mwombe Roho Mtakatifu akusaidie uweze kulielewa vema neno la MUNGU.
 
Me naomba kujua kwa hapa dar chakula haswa cha nguruwe ni nini na kinapatikana wapi kwa gharama kiasi gani.

Na kimahesabu nguruwe mmoja kwa mwezi anatumia chakula cha bei gani?

Mama yangu yuko njombe yeye analisha pumba. Ya mpunga anachanganya ya mahindi. Yule anaenyonyesha anapata ofa anamixiwa na mashudu ya alizeti.
 
Siku nyingine kabla ya kuanza biashara hakikisha una soko yaani unajua pa kuuza.
Dar kuna machinjio nyingi za nguruwe anzia huko.Pia instagram wanaofanya biashara za nyama wapo wengi na kurasa zao.
waweza wasiliana nasi tukupe connection
 
Siku nyingine kabla ya kuanza biashara hakikisha una soko yaani unajua pa kuuza.
Dar kuna machinjio nyingi za nguruwe anzia huko.Pia instagram wanaofanya biashara za nyama wapo wengi na kurasa zao.
waweza wasiliana nasi tukupe connection
Naomba connection
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] fuga Bata mkuu hawa hawana kelele kabisa
 
Uwekezaji mzuri sana huo. Gharama kubwa ni msosi wao. Hawauguagi hovyo wakitunzwa vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…