Nafanyaje Malipo AliExpress?

magallo

Member
Joined
May 31, 2016
Posts
46
Reaction score
24
Ndg ZANGU kwayeyote anaetumia mtandao wa AliExpress naomba kujulishwa namna ya kufanya malipo Kwa bidhaa itayofanyiwa order wao wanaelekeza nifanye Kwa card nami sinakadi ndio maana nauliza kama nawezalipia Kwa Mpesa ama mtandao wowote maana nimejaribu kuona namna yakufanya hayo malipo kwasimu sioni pahala.tafadhari pia naomba kujua credibility ya mtandao huu kama nitafanya order.
 
AliExpress ni mtandao salama na wala hauna kwere yoyote. Nimefanya a lot of transactions hapo.

Kufanya MALIPO ni simple kama kuteleza tu.

Kama una VODA tengeneza M-PESA visa card (zamani ilikua Master Card) au kama una AIRTEL tengeneza Airtel Visa Card

Utapewa Card Number, CVV, day of expiry.
Hiyo ukienda AliExpress utachagua kulipa kwa kadi utajaza taarifa zako chap . Yenyewe itakata MALIPO automatic


Kama una maswali zaidi nicheki
Whatsapp 0745090905
Calls- 0656400654
nitakusaidi mana kuandika maelezo mengi nayo kipaji
 
Umemaliza....ujengewe sanamu kabisaaaa
 
Hii convetion rates zake huwa kubwa. Utajikuta badala ya kutumia 50,000 unatumia 60,000!

Solution nzuri ni kufungua account ya USD tena kwa uraisi atumie stanbic
 
Kama una account ya benki inayotumia tzs omba benki waiwezeshe ifanye malipo online.

Ukiweza nenda benki kafungue acc ya dola, hapa stanbic wako njema maana current account zao hazina makato ya kijinga!!

NB: usijiloge utumie mpesa sijui tigopesa itakula kwako
 
Hii convetion rates zake huwa kubwa. Utajikuta badala ya kutumia 50,000 unatumia 60,000!

Solution nzuri ni kufungua account ya USD tena kwa uraisi atumie stanbic

Pia kuna benki zinatoa kadi za Visa na unaweza fanya malipo online mfano BankABC, UBA, GTBank...

Unaweka mpunga benki in TZS, si lazima akaunti iwe ya USD...
 
Kuna order nilikuwa nataka kuilipia Aliexpress, nilivoweka zile tarakimu za benki nikatakiwa kuweka CVV ,hapa kuna American express ambazo ziko tarakimu nne na local ziko 3, nikaweka tarakimu 3, lakini kila niki-allow inakataa nikaenda mpaka CRDB bado zoezi halikufanikiwa, Teller akaniambia niwasiliane na supplier anipe njia mbadala ya kufanya malipo, Nikamtafuta Mwalimu RTC akanielekeza hiyo ya MPESA VISA.

Lakini hitaji langu kubwa ni kutumia bank account. Tafadhali kama kuna mtu alishakutana na kadhia hii na akaitatua msaada tafadhali.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa 2factor authentication hizo nadhan hazina!!

Stanbic ndo mwisho wa matatizo.. kuna card yao inaitwa gold alafu uwe na acc ya current yani unakua unaserereka tu
Hiyo gold account ina monthly fees kubwa sana (sijui kwanini umeamua kutoeleza hiki kipengele)

Yaani iko hivi, hizi accounts za Gold (hata FNB wanayo) hawana makato ya kijinga (mfano kila unapo-withdraw pesa ATM).

Lakini wana makato fixed kila mwezi. Ni makubwa sana. Yanamfaa mtu mwenye mkwanja mrefu na transactions nyingi sana.
 
Binafsi sijawahi ona makato ya mwezi ila nadhan wananikata kwa miezi 3 au 6. Sina data kamili lakin ni acc ambayo naona haina makato ya kijinga. Tafadhali nenda kwao utapata muongozo au ingia google search "stanbic fees pdf" then download hiyo pdf uzisome.
 
Nashukuru sana ndg yangu Kwa ufafanuzi wako mzuri juu ya namna yakufanya malipo. Ntafuata maelekezo Yako nitengeneze Airtel visa card,nikifanya hivo tatizo litakuwa kwisha.shukrani sana .
 
Nashukuru Kwa mchango wako naona unawezekana kwani Nina account Stan Bic basi ntawaona Ili waiwezeshe account yangu kuweza kufanya malipo hayo .shukrani sana ndg yangu Kwa mchango wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…