Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,306
Nafasi ya Cheti kwenye Ajira
Miaka ya 1980s kurudi nyuma, hali ilivyokuwa ni kwamba serikali ilikuwa ikihitaji watumishi wengi, lakini waliokuwa na sifa ambazo serikali ilikuwa ikizitafuta, walikuwa wachache. Wanafunzi waliokuwa wakihitimu kidato cha nne, walikuwa na fursa za kuajiriwa moja kwa moja serikalini, kwenda vyuo mbalimbali, au kwenda sekondari ya juu.
Nini sekondari, wakati tunamaliza shule ya msingi baadhi ya wenzetu walichaguliwa kwenda vyuo kusoma...
Waliokuwa wakimaliza chuo kikuu enzi hizo, walikuwa ni wachache, huku kabla ya kuhitimu, wakiwa bado chuo kikuu, walipewa ofa za ajira na taasisi mbili tatu za serikali zilizokuwa zikiwagombania...
Miaka iliyofuata, hayo yakawa historia, kwa vile serikali haikuweza tena kuajiri kila mhitimu, kwa vile wahitimu walikuwa wengi, na nafasi zikapungua, hasa kutokana na kupungua kwa idadi ya mashirika ya umma.
Baadhi ya vijana, wanasonga kwenye safari ya elimu, wakiwa na dhana iliyofanya kazi zama zile za zamani ambazo ukionyesha cheti chako tu cha kuhitimu, unagombewa mithili ya mpira wa kona na taasisi zinazotaka kukuajiri.
Kwa sasa, siyo Tanzania tu, bali dunia nzima, wahitimu wamekuwa wengi, na baadhi ya taasisi zimeacha kuangalia vyeti, na badala yake kuangalia ujuzi na maarifa aliyonayo mtu.
Kule Nigeria kwenye wahitimu lufufu, waajiri wameacha kuangalia vyeti, na badala yake wanatoa mitihani ya aptitude kabla ya kufikiria kutoa ajira.
Google Announces Three New Tech Skill Certificates on Coursera, Offers 100,000 Scholarships for Enrolled Jobseekers - Nevada Business Magazine.
Kwa mfano, Google wametoa kozi ifuatayo, ambayo wenyewe wanaichukulia ni kama shahada ya miaka minne. Kozi hii unaweza kuisoma bure. Wewe tu na bando lako.
IT Support Certificate Training Program - Grow with Google
"Completing the program can earn you up to 12 college credits, the equivalent of 4 associate degree-level courses."
Ushauri wangu kwa vijana ni kwamba, usiende kwenye safari ya elimu kwa kutegemea kwamba utakapopata digirii yako mwisho wa safari, patakuwa na utitiri wa waajiri wakigombea wakuajiri, kama ilivyokuwa zamani. Hilo treni lishaondoka. Kwa sasa hivi tafuta ujuzi na maarifa ambayo yatalazimisha waajiri au wateja wakutafute. Ndiko tunakoelekea. Na ndipo tuliko tayari.