Nafasi ya Ushairi wa kuongea ‘spoken words poetry’ katika kuleta faraja na kuinua ari ya kutafuta ufahamu

Nafasi ya Ushairi wa kuongea ‘spoken words poetry’ katika kuleta faraja na kuinua ari ya kutafuta ufahamu

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Katika ulimwengu tulionao na kwa namna ya maisha tunayoishi ni wazi kuwa tuna muda finyu wa kujisomea mambo yenye hoja za msingi. Hali hii ni tatizo lakini kila jamii imejitahidi kutumia Sanaa na teknolojia kiujumla ili kuhakikisha kwamba watu wanapata mambo ambayo wangeyapata vitabuni.

Kupitia teknolojia, na kujua kuwa watu wana muda finyu wa kusoma, siku hizi imeanza mifumo ya kuweka vitabu katika mfumo wa video au sauti ili mtu aeze kusikiliza yote yaliyoandikwa kwenye kitabu huku akiendelea na shughuli nyingine

Uandishi wa vitabu ni mzuri lakini audio books zinafeli kwenye eneo la kushindwa kuwa na sanaa katika usomaji. Hapa ndipo inpoingia nafasi ya ushairi wa kuongea, ambayo kwa historia mashairi haya yalikuja ili kuwafanya watu wapate ujumbe kwa uzito wa ujumbe utolewayo, lakini pia mtu avutiwe na aburudike kusikia.

Ushairi wa kuongea, unaandikwa kwa uzito mkubwa hoja na maoni ambao sio lazima kufuata vina, kuwa na kiitikio nk, ila huwa na midundo ili kuwa na radha katika ghani zake.

Msanii wa Marekani Prince Ea, amewahi kueleza mafanikio yake mara baada kuamua kuachana na muziki wakufokafoka na kuingia kwenye mashairi akiwa inspire na ku-motivate watu wenye mambo tofauti tofauti

Pia yuko mtu mwenye PhD, Dr Cornel West ambaye naye anafanya spoken word poetry kwa nchini Marekani. Wasanii wa spoken word poetry wapo wengi kwa nchi zilizoendelea kuliko nchi za Afrika,

Tukijilinganisha na wenzetu wakenya sisi tuna wasanii wachache zaidi, wakiongozwa na bwana Mrisho Mpoto, Yupo bwana Justine Kakoko ambaye ana album mbili za ushairi, Uafrika ni Wajibu, na Duniani nyumbani. Yupo mwanadada Zuhura the lioness ambaye ana album ya Love blooms. Pia Male Hanzi amefanya mashairi kadhaa kwenye album yake ya hip hop alikuwa na track mbili za ushairi wa kuongea, Sababu ni moja na Kijiji cha kuku

Pia yupo Hellen Burugu ambaye ametamalaki Youtube kwa ngoma zake za ushairi wa kuongea. Pamoja na Amos Mwijonge

Ushairi wa kuongea unajali zaidi ujumbe kuliko vina, aina hii ya ushairi ni tofauti na ngonjera ambayo mara nyingi una namna moja ya ghani pia naziona ngonjera kama tambo za majigambo.

Katika huu ulimwengu ambao watu tuna matatizo mengi na tunahitaji faraja, lakini hatuna muda wa kusoma vitabu vya self help kutokana na ufinyu wa muda basi ni vyema kusikiliza mashairi kupata ujumbe ambao unaweza kuwa ni faraja au kupata hoja zinazoweza kuibua kiu ya kufahamu vitu ambavyo washairi wanaweza kuwa wamevizungumza katika kazi zao.

Teknolojia siku zote imekuwa msaada mkubwa kwenye kufanya maarifa yamfikie mwanaamu, tangu ugunduzi wa maandishi, ungunduzi wa wino, karatasi, printing press, computers na mambo mengine ambayo hufanya mtu kupata taarifa au maarifa

Signed: Oedipus

=====


Justine Kakoko



Zuhura


Malle Hanzi



Hellen Bulugu



Amosi Mwijonge
 
Mkuu Mrisho Mpoto aka Mjomba ndio gwiji wa hii fani katika ukanda huu!!!
 
Huko mbele. Kuna watu wanaitwa Hiphop preachers, ni hatari. Prince ea, naye yupo vizuri Sana.

Lakina pia kuna motivational speakers, siongeleei hao wanaofanya kwa kushibisha tu, wale ambao wana Sauti za ndani, ukiwasikia unakula ujumbe na Burudan.

Ukikutana na madini ya ET. ERIC THOMAS, LESS BROWN etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom