Pre GE2025 Nafasi ya ushiriki kwa Wanawake wa vijijini katika katika kuwania nafasi za uongozi uchaguzi wa Serikali 2024

Pre GE2025 Nafasi ya ushiriki kwa Wanawake wa vijijini katika katika kuwania nafasi za uongozi uchaguzi wa Serikali 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wanajukwaa Kwema!

Siku zinahesabika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajiwa kufanyika November 27 mwaka huu nchini kote.

Sasa swali la kujiuliza vipi muamko wa Wanawake wa vijijini kushiriki katika kuwania nafasi hizo ambapo mara zote kumekuwa na muhamko mdogo sana wa kuthubutu kuchukua fomu ndani ya vyama vyao vya kisiasa na kwenda kusimama kwenye majukwaa na kunadi sera zao mbele ya wananchi ili wapate nafasi za uongozi.

Ukizidi kuangalia kiujumla wanawake wamekuwa na muitikio mdogo sana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na wengine wakifika mbali na dhana potofu kuwa wanawake awana uwezo wa kuwa viongozi bora. Jambo ambalo binafsi naona si lakweli.

Ukitazama uthubutu kwenye uduchu wa wanawake wa mjini wamekuwa kidogo wanajitokeza na kuleta ushindani mkubwa kwa wanaume katika kugombea nafasi za uongozi wa taifa au ndani ya chama chake cha siasa ukilanganisha na wanawake wa vijijini ambao wamekuwa waoga na mfumo dume ambao umeendelea kutumika zaidi baadhi ya maeneo ya vijijini.

Sasa ni wakati sahihi kwa wanawake wa maeneo ya vijijini wenye uwezo na wenye kukidhi vigezo vya ugombea waanze mchakato sasa wakwenda kuchukua fomu za kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Lakini naona pia Vyombo vya habari vinaweza kusaidia kuleta uhamasishaji kwa kuonyesha simulizi za wanawake waliofanikiwa, kutoa habari za motisha na fursa kwa wanawake wa vijijini. Matumizi ya redio za kijamii na mitandao ya kijamii vinaweza kufanikisha uhamasishaji huu.
Vipi na wewe mdau unamaoni gani kwenye hili?
 
Ushiriki wa wanawake katika uongozi ni muhimu kwa maendeleo ya jamii.
Kuna njia nyingi za kuhamasisha wanawake wa vijijini kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
  • Elimu: Kutoa elimu kwa wanawake kuhusu haki zao za kisiasa na umuhimu wa ushiriki wao katika uongozi.
  • Uhamasishaji: Kufanya mikutano na semina za kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea.
  • Usaidizi wa kifedha: Kutoa msaada wa kifedha kwa wanawake wanaotaka kugombea ili kuwasaidia katika kampeni zao.
  • Utetezi: Kufanya utetezi kwa wanawake ili kuhakikisha kwamba wanapata nafasi sawa na wanaume katika uongozi.
 
Back
Top Bottom