ALLAN MAKALA
New Member
- Sep 12, 2023
- 1
- 0
MAPAMBANO KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA KUREJESHA MAADILI KATIKA JAMII.
Imekuwa kama hadithi ya kuzoeleka katika jamii, watu wakifanya matukio ya kutisha kila kukicha hapa nchini. Wengine huwa tukiamka asubuhi tunaangalia taarifa za jamii zilizoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya hapa nchini ambapo hazijawahi pita siku zaidi ya tatu hatujasikia matukio ya ajabu kama ulawiti, ubakaji, mauaji ya wanandoa na mengine mengi kwenye jamii.
Imenisikitisha sana kuandika hivi, Matukio mengi ya unyanyasaji kwa Watoto wakike kwa wakiume hutokea majumbani kwao au kwa ndugu zao wapendwa ambao pengine wangekua chanzo cha maarifa na maadili mema kwa Watoto hao! Vivyo hivyo tunasikia pia hata wale waliohalalishwa kua mwili mmoja kwenye nyumba za ibada wakigeuka kua wauaji wakubwa kwa wenza wao na wanafamilia wenzao!
Kiukweli kuna mwamko mkubwa wa jamii dhidi ya suala hili pia serikali inajitahidi vilivyo kutokomeza suala hili ikishirikiana na jamii pia vikundi binafsi vya haki za binadamu, lakini bado tunasikia matukio haya na hivyo basi kupitia jamii forums stories of change ninawasilisha mawazo yangu ambayo hayajatoka akilini tu bali hata moyoni kwakua ninaumizwa sana na vitendo hivi.
1. Ukaribu na urafiki kwa Watoto uongezwe na isiwe tu ni kazi ya mama au mwalimu wa daycare bali na Baba asimame imara. Wazazi wengi katika hizi zama wamekua wakijiweka mbali sana na Watoto wao wanafikiri majukumu ni kumnunulia mahitaji mtoto na kulipa ada, hapana hii haitoshi inahitajika mzazi asimame katika kila kona mwanae anapopatikana au aweke mazingira ya urahisi ya upatikanaji wake mtoto anapomuhitaji tena bila vipengele vyovyote. Ukaribu kwa mtoto unamjengea kujiamini na shauku ya kujieleza mbele ya mzazi juu ya mambo yaliyotokea ambapo ataweza kuripoti hata vitendo viovu alivyovishuhudia au kufanyiwa bila kuficha kama inavyotokea kwenye jamii ambapo unakuta mtoto ameanza kukatiliwa tangu miaka miwili iliyopita na inakuja kugundulika akiwa tayari katika hatua mbaya. Ukaribu kwa mtoto unajengwa kwa njia nyingi sana ikiwemo, kushiriki nao katika michezo yao ambapo inawasaidia wao kumuona mzazi kama mwenzao na kumzoea Zaidi bila kumuogopa, Pia mzazi anaweza kutenga muda kabla ya watoto kulala kuongea nao bayana (Privacy) juu ya mambo wanayopitia itamuwezesha kukuamini zaidi, ila pia mzazi anaweza kujenga tabia ya kuambiana siri na mtoto ili nayeye aone kwamba kumbe hata wazazi wana siri zinazowasumbua na hapo mtoto atafunguka vyema, siri za mzazi si lazima ziwe nyeti hapana inaweza ikawa siri hata ya wakati na yeye bado ni mtoto au zenye faida mfano kumwambia kua umewahi kula mandazi ya wageni utotoni. Pia mzazi ataboresha uhusiano na mtoto wake pale ambapo atatenga muda kuwachunguza marafiki wa karibu wa mtoto wake shuleni na nyumbani na itarahisisha kufichua uovu (follow up).
2. Kama mzazi inabidi kuchunguza na kuchagua vipindi vizuri vya kuangalia Watoto kwenye runinga au hata mitandaoni. Watoto hujifunza kwa njia nyingi sana hasa za burudani kama michezo au vipindi vya runinga, ukweli ni kwamba maudhui mengi mabaya na maovu yanarushwa Zaidi ya yale maudhui mema mfano movie na miziki mingi sana nahakika hili linajiekeza vyema, hivyo ni vizuri kama mzazi au mlezi kutenga muda wa kuchagua vipindi au movie zenye maudhui mazuri kwa Watoto, mfano kufanya review ndogo ya movie ili kuchunguza na pia mzazi anaweza kununua flash ambayo atazitunza zile movie au katuni safi ili kupunguza Watoto kuangalia maudhui mabaya ikiwemo picha za ngono. Mtoto anaweza kusikia au kuambiwa jambo Fulani lenye kukiuka maadili na pia akaja kuliona kwenye runinga au mtandaoni atajenga dhana kwamba hilo jambo ni sahihi sema wazazi wananibania tu, hivyo kama kuna uhitaji wa kumweleza kua jambo hilo ni baya basi njia sahihi zitumike.
3. Kweli Jukumu la malezi ya mtoto ni la jamii nzima ila lianze na mzazi kwanza alafu ndo waje wengine, hivyo Mzazi asimwamini kila mtu katika malezi ya mwanae maana wapo wenye nia mbaya watakao muumiza mtoto. Ifike hatua tukubali kua kwenye jamii yetu wapo watu wazima kwa vijana wenye maadili mabaya ambao ndio hao wanaofanya ukatili, Cha ajabu wengi ni ndugu au jirani wa karibu kabisa. Hivyo mzazi usiweke Imani ya moja kwa moja kwa jirani au mgeni hata kama ni ndugu mnafahamiana kwa muda, ikumbukwe watu hubadilika! Kwaiyo inabidi chumba cha kulala Watoto kisifikiwe na mtu mwingine kirahisi ikiwezekana mzazi atafute namna ya mgeni kulala bila kuwaathiri Watoto maana kumuweka mgeni sjui binamu, mjomba au baba mdogo kulala na Watoto kumeibua kesi nyingi sana za ulawiti na ubakaji na inaumiza kwakweli maana nimewahi kulishuhudia tukio la namna hii. Hivyo mzazi ni vyema kuchunguza watu wanaokua karibu na mtoto wako pale ambapo haupo ikiwemo wafanyakazi wa ndani, ndugu, jirani na wengine bila kujali mionekano wala wadhifa wao.
4. Kuwafichua wanaofanya ukatili bila kuwaogopa na kuwaripoti kwenye vyombo vya dola. Eti kisa ni mtoto wa mtu mkubwa, au yeye mwenyewe ni mkubwa au ni ndugu basi kumstiri ni kuficha maovu yake, hapana jamii itambue kwamba kuwaficha watu kama hao ni kufuga simba ambaye atakuja kukutafuna mwenyewe akikua. Hivyo haki itendeke bila kusuasua, uzuri ni kwamba serikali inalishughulikia swala hili barabara! Ikishilikiana na vyombo vya dola na madawati ya kijinsia.
Kiujumla mzazi anachangia zaidi ya asilimia 90 kwenye kutunza na kutengeneza jamii yenye maadili mema kupitia malezi bora ya mtoto kikubwa ni kutambua nafasi yako na kutenga muda kiasi kwa Watoto nah ii itapunguza au kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya Watoto. Elimu inamchango mkubwa sana kwenye kutokomeza ukatili kama huu, Hivyo wazazi kwenye jamii waelimishwe au wakumbushwe ili waongeze bidii kutokomeza maovu kama haya na hii inawezekana kupitia program mbalimbali zinazoanzishwa na serikali au mashirika yasiyo ya kiserikali.

Upvote
0