Tuache mambo ya hearsay wakubwa, mbona watu wanaomba vibarua hivyo na wanapata hata bila Zengwe la kihivyo....yes, inawezekana kuna watu wameshapata mizengwe hiyo lakini si kweli kuwa kazi zote za serikalini zina zengwe....si kweli!
Mi binafsi, sina hata balozi wa mtaa ndugu yangu....nishaombaga kazi nyingi serikalini, kuna baadhi nilikosa na nyingine nikapata...mfano nilipata pale TRA, Economic Empowerment Council, Tanesco (hapa kidogo palikuwa kazengwe),Kule magogoni-Utumishi, Hazina........! Hizi sehemu nilizopata naamini ni kwa sababu ya sifa nilizokuwa nazo na si vinginevyo, na huko nilikokosa naamini kulikuwa na ushindani na nilishindwa kwa kuwa kulikuwa na watu wengine waliokuwa na sifa zaidi ya mimi.
Hata huko BOT mbona kuna washikaji kibao wanaomba kazi pale from UD, IFM etc na wanapata?
Kabla hatuja lalamika eti, kuna upendeleo or sijui wameshapata watu, wewe unayetaka nafasi iliyotangazwa jiulize kwanza una sifa wanazotaka? je, Una First au Second Class from Accredated university? una age below 30yrs if yes, omba hiyo job....then ukikosa njoo utwambie umekosa, na ufanye uchunguzi wale waliopata wanasifa gani, then tunaweza kuwa na hoja ya upendeleo/rushwa etc!