huyo mdogo wako ni he au she?
Ni HE. Alisoma SUA mifugo na baadaye akabadili kabisa field. Akaenda kusomea sheria akakatiza. Akafanya kazi kwa muda ili kuvuta muda na baadaye akaacha na kwenda SUA. Sasa hivi ninaposema yeye ni Mwalimu wa SUA tayari.
Ingelikuwa miaka ileee, ningelisema ni Marehemu dada yangu kamfanyia mpango. Ila sasa hivi kwenye familia ni YEYE anawafanyia watu mipango. Ila katika ile anga, hata yeye alikuwa PEKE YAKE.
Ila kilimsaidia ni kitu kimoja. Hilo somo atakalofundisha, SUA walikuwa hawana Mwalimu. Walijitahidi kumlima maswali ya sehemu tofauti tofauti. Ila hawakufahamu kuwa jamaa pamoja na kusomea Mifugo, alikuwa pia kafanya kozi chuo cha ushirika Moshi na akasomea sheria hadi sijui mwaka wa pili. Sasa kila wakitaka kumkamata, aliwapeleka kwenye mambo ya SHERIA ambako walimu wengi wa SUA hawana mwanga na huku akitoa au kutumia mifano mambo ambayo SUA wako mbioni kuyafanya ila hawaelewi vizuri ni kitu gani. Kwa haraka haraka nisema kwamba aliwaacha kwenye mataa na ikabidi tu wampe nafasi.
Sasa kukata tu tamaa vila kujaribu si sawa. Unaweza kuwa kama mdogo wangu na wewe ukachaguliwa. Kabla hajapata kazi SUA, alikuwa hajawahi kwenda Ulaya hata siku moja. Kasoma na kumaliza shule na vyuo vya Tanzania. Wanaotoka Ulaya nafikiri kinawasaidia ni KUJIAMINI. Wakirudi Tanzania huwa wanajiamini kupita kiasi. Sasa aliyemaliza SUA sijui UDSM akiwaona hao Maprofresa au Madokta anaanza kutetemeka. Hii naisema kwa kutumia uzoefu wangu mwenyewe. Tangu nirudi Tanzania, naongea na kila aina ya msomi/tajiri bila ya kujali yeye ni NANI. Complex imeisha kabisa. Na kama sikosei mdogo wangu hii kitu pia anayo. Hana complex kwa mtu yeyote na labda ni mazingira aliyokulia.
Jamani mkienda Interview, msihofu kabisa. Fanya kama vile unafahamu kuwa HUPATI. Utakuwa more relaxed na kujiamini sana. Ukifanya kwa imani "LAZIMA NIPATE" hiyo ndiyo huwa inaanza kuleta wasiwasi "ila nikikosea ndiyo basi". Tujiamini na milele ujifunze kusema "liwalo na lile", mlango mmoja ukifunga, mingine 10 inafunguka na mwisho "mgaa gaa na upwa, hali wali mkavu. Pigania ila ukikwama, usikate tamaa, life goes on.