Nafasi za kazi ya dereva wa mitambo daraja II, Halmashauri ya mji Geita

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
4,876
Reaction score
1,549
TAREHE: 26/05/2020 YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA DEREVA WA MITAMBO DARAJA II – NAFASI 3

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita anawatangazia nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa waombaji wenye sifa za kujaza nafasi za uendeshaji wa mitambo ya “Roller, Excavetor na Grader” kama ilivyoorodheshwa katika tangazo hili;-

1.0. MAJUKUMU YA KAZI
Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa dereva mitambo mwenye uzoefu.
Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa.

2.0 SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
  • Kuajiriwa mwenye leseni ya daraja G ya uendeshaji Mitambo.
    NB: Wenye leseni zenye sifa za ziada kama daraja F, E na C1 watapewa kipaumbele.

3.0 MASHARTI YA JUMLA
  • Awe raia wa Tanzania.
  • Awe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (Detailed CV) yenye anuani ya Posta na namba ya simu ya kuaminika ikiambatana na majina ya wadhamini watatu (3).
  • Maombi yaambatanishwe na nakala za cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo ya uendeshaji wa mitambo na vyeti vya kidato cha Nne vilivyodhibitishwa na Mwanasheria.
  • Muombaji aambatanishe picha ndogo ya rangi (passport size) ya hivi karibuni.
  • Testimonials, Provisional results, Statement of results na hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (form VI and form IV result slips) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma elimu ya kidato cha nne (4) nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA).
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya kazi kwa waajiri wao.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa Kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
4.0 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya mshahara TGOS A kwa mwezi.

5.0 UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15/06/2020 saa 9:30 alasiri. Maombi yatumwe kwa njia ya Posta kwenda kwa Mkurugenzi, Halmashauri ya Mji, S.L.P 384 GEITA. Waombaji watakaokidhi vigezo watajulishwa kwa njia ya simu na matangazo ili kuweza kuja kwenye usaili.

Eng. Modest J. Apolinary,
MKURUGENZI,
HALMASHAURI YA MJI, GEITA.
 
wenye sifa za kujaza nafasi za uendeshaji wa mitambo ya “Roller, Excavetor na Grader”
Kaka! Umeonesha aina ya kazi na siyo aina ya ajira.Ninachotaka kujua ni kama ajira hii ya kudumu au ya muda maalumu?.
 
Wanataka plant operators au waendeshaji Wa mitambo?!

Maana ku-operate Na kuendesha (driving) nivitu viwili tofauti!
 
Back
Top Bottom