Nafasi za kazi za kumwaga ILOVO Kilombero Sugar.

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Posts
5,551
Reaction score
2,153
Uongozi wa Kampuni ya ILOVO Kilombero Sugar Ltd. unayo furaha ya kutangazia UMMA kuwa msimu wa kukata Miwa umeanza rasmi.
SIFA ZA MUOMBAJI:
Awe na tabia njema
Awe na afya njema.
Awe na Bidii.

PACKAGES:
Ukipata kazi utarudishiwa nauli ya Basi au Treni iwapo tu utawasilisha risiti au tiketi.
Pesa itatolewa kwa siku(Target based)
Nyumba na usafiri wa kwenda na kurudi shambani (Hasa yaliyopo mbali) ita/utatolewa.
Wale waliofanya kazi msimu uliopita na kupata HATI SAFI watafikiriwa kwanza.

Shime Wananchi kama unajua jamaa/Jirani/Masela zako wanaolalamikia Ajira nafasi ndiyo hiyo.
 

Mambo ya kilimo kwanza hayo
 
Yeah AJIRA hizi hazihitaji elimu... ni NGUVU tu... Binafsi naupongeza sana uongozi wa KILOMBERO SUGAR kwa kutangaza ajira kama hizi nzima,tofauti na Makampuni mengine ya kuhusisha kazi za nguvu kutoa ajira kwenye maeneo yanayowazunguka ambalo kupelekea kudhani wa-TZ ni wavivu saaana!
 
vijana wa siku hizi wanataka dasilamu yani hata wawe wafagia vyoo na digrii lakini wawe tu dar
 
vijana wa siku hizi wanataka dasilamu yani hata wawe wafagia vyoo na digrii lakini wawe tu dar

jamani kama hamna cha kusema humu JF, ni bora uchukue jembe ukalime, sasa digrii na kusafisha vyoo? Kweli? Tuwe serious.
 
Yeah 2we serious guys! Mkuu asante kwa taarifa,nina jamaa yangu anastrugle sana na kwa vile hana elimu ngoja nimpe taarifa. Vp wanalipaje kama waweza kutusaidia pia? Maana m2 wa mbali inabidi awe na taarifa ajue opportunity cost.
 
Unapataje hiyo kazi? I mean, links kwaajili ya kufanya maombi, anuani, any possible contact, deadline and more details. Nataka nikatumie akili na muda wangu kwaajili ya hizo kazi, for now niko mjini Dar when i get to know kila kitu nitapanga safari ya kufuata job badala ya kukaa nyumbani idle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…