Nafasi za ku-volunteer?

Mgombezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Posts
610
Reaction score
181
Wana Jamii, Naomba kwa yule ambae ana nafasi katika ofisi yake au sehemu yeyote ambayo unafikiri unaweza kuweka vijana wakafanya kazi kwa kujitolea (kama utaweza kuwawezesha nauli tu na mlo wa mchana itakuwa vyema).

Naomba uni-PM, ukieleza jina la ofisi/kampuni; unahitaji mtu wa ku-volunteer katika eneo gani?, mahali ulipo (mkoa, wilaya...)

Kumbuka hawa volunteer wengi watakuwa wamemaliza kidato cha 4 au 6, hawana ujuzi hivyo watahitaji maelekezo kidogo katika eneo utakalompangia. Waitaweza kutumika kati ya mwezi 1 - 3, utaweza kueleza unamhitaji kwa muda gani.

Nafikiri wataweza kutenda katika maeneo ya huduma kwa wateja, kutafuta masoko, mhudumu wa ofisi, ufundi - kumsaidia fundi, viwandani, na sehemu nyinginezo ambazo hazihitaji ujuzi.

Natanguliza shukrani kwa ushirikiano wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…