Tcu wanamfumo mbovu sana! Ila ndugu kaangalie hata kwenye jeshi la wananchi wa tz! Unaweza pata kazi!
Wana JF
Mimi ni mmojawapo wa watu waliomaliza Diploma mwezi June mwaka huu, na mpaka matokeo yanatoka tayari muda wa kuomba kupitia mfumo wa CAS, ulioendeshwa na TCU ulikuwa umepita, sasa napenda kuwauliza wadau kama kuna mtu ana taarifa za sisi kupewa nafasi nyingne ya kuomba kujiunga na masomo ya shahada mwaka huu.
naomba mwenye taarifa anijuze maana mtaani hakufai ni bora kurudi shule kuongeza elimu.
fuatilieni vizuri yaani kila kitu walieleza kwenye website yao na watu wakaelewa kabisa sijui mkuu uliona uvivu kuperuzi? kwa wanafunzi waiomaliza diploma matokeo yao yalikuwa yanatoka kabla ya mwezi wa tano wanaweza kuomba kusoma kupitia TCU ila wengine woote watakaomaliza baada ya hapo watasubiri mwakani kuomba kupitia TCU tangazo hili lilkuwepo kwenye website ya TCU toka february 2012. nilikuwa nafuatilia hili maana kuna mdogo wangu huko nae amemailza diploma ndio nikayajua haya.
mkuu UKI nilisikia watu wenye diploma wanaotaka kuapply vyuo walitakiwa wakavisajili vyeti vyao NACTE. je,uliisikia hii taarifa?