Jamani, wale wataalam wa afya kama Dental Therapists na Clinical Officers wanataka kusoma ADO au AMO mwaka huu wasibweteke kuomba shule Kusoma ADVANCED DIPLOMA.
Application zote zipo kupitia website ya NACTE. Naambiwa inaenda hadi July maombi hayo yatatapofungwa. Tafuta kozi unayotaka kutokea hukohuko kuliko kwa walioko kazini au mwenye jamaa yake anayetaka kuongea value ya utumishi wake.
Kwa DT tafuta ADVANCED DIPLOMA IN CLINICAL DENTISTRY. Kwa Clinical Officers tafuta kozi ya ADVANCED DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE.
Kisha fuata maelekezo. Au wasiliana nao kwa anuai walizoweka hapo.