Nafasi za mafunzo maalumu ya uakimu

Nafasi za mafunzo maalumu ya uakimu

MAULA

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,056
Reaction score
170
TANGAZO LA NAFASI ZA
MAFUNZO MAALUMU YA
UALIMU TARAJALI NGAZI
YA STASHAHADA -
SAYANSI NA HISABATI
|
Print |
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO
MAALUMU YA UALIMU TARAJALI
NGAZI YA STASHAHADA KWA
MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI
KWA MWAKA WA MASOMO
2014/2015
Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, anatangaza nafasi
za Mafunzo Maalumu ya Ualimu
Tarajali Ngazi ya Stashahada kwa
masomo ya Sayansi na Hisabati.
Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea
uwezo washiriki katika taaluma ya
masomo mawili ya kufundishia katika
shule za Sekondari. Mafunzo haya
yatafanyika kwa utaratibu ufuatao:
(i) Watakaochaguliwa watapatiwa
mafunzo ya miezi mitatu ili
kuimarisha taaluma ya masomo ya
Sayansi na Hisabati waliyosoma katika
Kidato cha Tano na cha Sita. Mwisho
wa mafunzo haya, washiriki watafanya
Mtihani Maalumu kwa lengo la
kutathmini uwezo wao (competence)
katika masomo tajwa.
(ii) Watakaofaulu Mtihani wa
mafunzo haya watajiunga na
mafunzo ya ualimu ya kawaida Ngazi
ya Stashahada kwa miaka miwili
kuanzia mwezi Julai 2014.
SIFA ZA WAOMBAJI
Waombaji wawe wamehitimu Kidato
cha Sita kati ya mwaka 1998 na 2013
na kufaulu kwa kiwango
kisichopungua ‘Subsidiary pass’
mbili katika tahasusi za PCB, PCM,
PGM, CBG, CBA na CBN.
MAELEKEZO MUHIMU
(i) Waombaji wa mafunzo ya Ualimu
watume maombi ofisi za Maafisaelimu
wa Mikoa au Wilaya; au watume
maombi yao kwa njia ya posta
yakionesha anuani zao (za posta, au
anuani ya barua pepe na simu);
pamoja na nakala za vyeti vya ufaulu
wa Kidato cha 4 na cha 6;
(ii) Majibu kwa watakaochaguliwa
kujiunga na mafunzo haya yatatolewa
kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz ;
OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz ;
na katika mbao za matangazo
Wizarani, ofisi za Maafisaelimu wa
Mikoa na Wilaya;
(iii) Barua za kujiunga na mafunzo
kwa watakaochaguliwa zitatolewa na
vyuo watakavyopangwa kwa kutumia
anuani zao; na
(iv) Tangazo hili lipo pia katika tovuti
ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi: www.moe.go.tz ; OWM-
TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na
kwenye mbao za matangazo Wizarani,
Maafisaelimu wa Mikoa au Wilaya; na
Vyuo vya Ualimu.
Maombi yatumwe kwa anuani
ifuatayo:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA
UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM (Aione:
Mkurugenzi, Idara ya Elimu ya Ualimu )
MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA
MAOMBI NI TAREHE 28/02/2014.

Mwambie na mwenzio
 
[h=2]Nafasi za mafunzo maalumu ya uakimu[/h][h=2]uakimu Are you serious..?![/h]
 
Back
Top Bottom