Nafasi za Masomo

kibunange

Senior Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
165
Reaction score
148
KUANZISHWA KWA FANI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA MSINGI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa - SEKOMU (zamani SEKUCo) kilichopo Lushoto, anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo mwezi Julai na Oktoba 2015 kwa Kozi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi yaani Diploma in Primary Teacher Education (DPTE).

A.SIFA ZA KUJIUNGA:

1.Waalimu Walioko Kazini (In-Service Candidates):
Muda: Miaka Miwili (2)
Sifa za Kujiunga: Alama za Ufaulu "D" NNE (4) au zaidi za Kidato cha Nne
NA

Astashahada ya Ualimu Daraja la III A iliyotolewa na NACTE au Mamlaka nyingine inayotambuliwa hapa nchini
AU Astashahada nyingineyo iliyotolewa na Chuo kinachotambulika hapa nchini
AU Stashahada nyingine iliyotolewa na Chuo kinachotambulika hapa nchini
NA

Uzoefu wa kazi ya kufundisha Shule ya Msingi kwa muda usiopungua miaka miwili.
2.Watarajali (Pre-Service Candidates) Ambao Wana Kidato cha Sita:

Muda: Miaka Miwili (2)
Sifa za Kujiunga: Alama za Ufaulu "Principal Pass" (E) MOJA (1) na "Subsidiary" (S) MOJA (1) au zaidi za Kidato cha Sita katika Masomo ya Lugha (Languages) au Sayansi ya Jamii (Social Sciences) kwa waliomaliza kabla ya 2014
AU

Alama za Ufaulu "Subsidiary" (S) MBILI (2) au zaidi za Kidato cha Sita katika Masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia, Baiolojia, Jiografia na Hisabati) kwa waliomaliza kabla ya 2014
AU

Alama za Ufaulu "Pass" (D) MOJA (1) na "Unsatisfactory" (E) MOJA (1) au zaidi za Kidato cha Sita kwa waliomaliza 2014 au baadaye katika Masomo ya Lugha (Languages) au Sayansi ya Jamii (Social Sciences)
AU

Alama za Ufaulu "Unsatsifactory" (E) MBILI (2) au zaidi za Kidato cha Sita kwa waliomaliza 2014 au baadaye katika Masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia, Baiolojia, Jiografia na Hisabati).
3.Watarajali (Pre-Service Candidates) Ambao Hawana Kidato cha Sita:

Muda: Miaka Mitatu (3)

Sifa za Kujiunga: Alama za Ufaulu "D" NNE (4) au zaidi za Kidato cha Nne.
B. UTARATIBU WA MAFUNZO:

1.Wanafunzi wa Masaa Maalum:

Kutakuwa na utaratibu wa mafunzo ya jioni Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 9.30 alasiri na Jumamosi kuanzia saa 3.00 asubuhi. Kozi itaanza kutolewa Lushoto na Tanga mjini. Watakaojiunga kwa utaratibu huu watakuwa Wanafunzi wamasaa maalum (Part-time students).
2.Wanafunzi wa Masaa Yote:

Kutakuwa pia na wanafunzi wa masaa yote (Full-time students). Mafunzo haya kwa sasa yatatolewa Lushoto na Tanga mjini.
Katika siku za usoni, Chuo kitaweka utaratibu wa kufundisha Kozi hii katika vituo mbalimbali ndani na nje ya Wilaya ya Lushoto.
C.UTARATIBU WA KUOMBA KUDAHILIWA:

Fomu za Maombi ya Kujiunga zinapatikana kwenye Tovuti ya Chuo ambayo ni Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU) na Tovuti ya Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (DKMs) ya KKKT ambayo ni www.elct-ned.org. Pia fomu zinapatikana SEKOMU Magamba, Kituo cha Mafunzo cha Tanga (Tanga Centre) kilichopo eneo la Usharika wa Kana uliopo Tanga mjini, Maktaba ya SEKOMU iliyopo Bumbuli Hospitali, Ofisi za Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Tanga na Sharika zote za DKMs.
Ada ya Fomu ya Maombi ya Kujiunga (Application Fee) ni TZS. 20,000 ambazo zinatakiwa kuingizwa katika mojawapo ya Akaunti zifuatazo:
NMB: SEKOMU A/C No. 4163300065
CRDB:SEKUCo UJENZI A/C No. 0150098857103
"Pay-in slip" ya malipo iambatanishwe na Fomu ya Maombi ya Kujiunga na kutumwa kwa:
REGISTRAR,
SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY,
P.O. BOX 370,
LUSHOTO.
Kwa wale wanaotaka kujiunga na mafunzo mwezi JULAI, siku ya mwisho ya kurejesha Fomu ya Maombi ya Kujiunga ni tarehe 15 Julai 2015. Mafunzo yamepangwa kuanza tarehe 25 Julai 2015.
Kwa wale wanaotaka kujiunga na mafunzo mwezi OKTOBA, siku ya mwisho ya kurudisha Fomu ya Maombi ya Kujiunga ni tarehe 15 Septemba 2015. Mafunzo yataanza tarehe 5 Oktoba 2015.
D. ADA:

Ada (Tuition Fee) kwa mwaka mmoja ni TZS. 800,000/=.
Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu 0685045067 au 0712 811420.
"PATA MAARIFA, TUMIKIA KWA UPOLE

CONTACT US

Sebastian Kolowa Memorial University,
P.O.Box 370,
Lushoto - Tanga,
Tanzania.

con tel (+255) 272977003
con fax (+255) 272977004
emailButton admin@sekomu.ac.tz

Registration Office

con tel (+255) 272977007
emailButton registrar@sekomu.ac.tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…