Nafasi za ualimu ordinary diploma

Nafasi za ualimu ordinary diploma

layoni

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2014
Posts
217
Reaction score
92
Ndugu wanajamiiforum;
Nimepitia kwenye website ya 'MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING' pamoja na ile ya NACTE nikakutana na majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kozi za ualimu ordinary diploma ambao wanatakiwa kuanza kuwasili sehemu husika walikopangiwa leo tarehe 01-06-2015.

Naomba tafadhali msaada kwa wadau wenye kujua hili kama kuna kuna awamu nyingine ya kutuma maombi ndani ya mwaka huu ili nasi tuweze kutuma maombi kwani nimemaliza mwaka jana 2014 kidato cha NNE na kufanikiwa kupata GPA 1.3 PASS. Kwa matokeo hayo ni wazi kabisa sitapata nafasi kidato cha tano hivyo nikafanya uamuzi wa kutuma maombi ualimu ingawaje jana nilipoingia website ya MoEVT na NACTE nikakutana na tangazo hilo.

Please nahitaji sana msaada wenu kama kuna nafasi tena ya kutuma maombi mwaka huu na MUNGU atawabariki.

Nawatakia kazi njema ya ujenzi wa taifa la JMT.
 
Nafasi ipo na wakati wa kuomba ndo huu. Ingia nacte na download tangazo la application 2015/16
 
NendA cafe zilizoko karibu nawe , mambo ya kuzingatia ni elf20 kwa m_pesa na elf5; kulipia cafe kingine zaid labda utaulizwa email kama unayo!; nk
 
Nashukuru sana wadau kwa mchango wenu
 
aixee mie nina crdit 2 vp wadau hapo ualim naenda mxaada jaman plz wana jf
 
Back
Top Bottom