Nafasi za waalimu tarajali Diploma. Imekaaje hii?

ipogolo

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
6,280
Reaction score
5,979
Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 12 Agosti 2013, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walitoa tangazo la nafasi za mafunzo maalumu ya ualimu tarajali ngazi ya stashahada(diploma) katika masomo ya sayansi na hisabati.
Mwisho wa kupokea maombi ilikuwa tarehe 20 Agosti 2013.
Kinachoshangaza ni kuwa waombaji wanaoishi Dar es Salaam , na mikoa jirani wapeleke barua zao kwa mkono na kuweka katika kisanduku kilichopo mapokezi.
Gharama ya kupanda basi kutoka mikoa jirani hadi dsm kwa watoto wa kawaida maskini huo sio unyanyasaji kiuchumi kisaikolojia na kijamii?
Kwani Shirika la Posta Limefungwa na halisafirishi barua ambapo ninaamini gharama haitazidi shs 1000/?.
Wizara niwaombe kwa niaba ya watanzania makabwela mtufikirie kuturuhusu kutuma maombi kwa njia ya posta.
 

we uko mkoa gani?
 
we uko mkoa gani?
Morogoro. Nauli ya basi ni zaidi ya shilingi 10,000/= jumlisha masaa 6 ya kusafiri hadi Ubungo na kurudi Moro. Masaa matatu ya kutoka Ubungo hadi wizarani na kurudi tena ubungo kupanda abood au lolote kurudi morogoro.
 
Morogoro. Nauli ya basi ni zaidi ya shilingi 10,000/= jumlisha masaa 6 ya kusafiri hadi Ubungo na kurudi Moro. Masaa matatu ya kutoka Ubungo hadi wizarani na kurudi tena ubungo kupanda abood au lolote kurudi morogoro.

kumbe moro dar ni 10,000! masaa 6 km 100 na... masaa ma3 ubungo hd wizara=masaa 9 ndo serikali yetu hii,jipange
 
Mleta mada kasome vizuri tangazo, mm nililisoma nikalielewa, ilikuwa kama uko dar na mikoa ya jirani upeleke kwa mikono na wamikoa ya mbali waliruhusiwa kutuma posta. Mdogo wangu alituma posta
 
Mleta mada kasome vizuri tangazo, mm nililisoma nikalielewa, ilikuwa kama uko dar na mikoa ya jirani upeleke kwa mikono na wamikoa a mbali waliruhusiwa kutuma posta. Mdogo wangu alituma posta

Nimelisoma nimelielewa. Wangesema kwa wansokaa dar lakini ukisema mikoa ya jirani sio haki MDHT.
Mikoa jirani ni pamoja na morogoro, pwani, lindi mtwara hata zanzibar.
MDHT kweli ni sahihi kutumia masaa 10 kwa kitu ambacho ningepost nikalipa buku nikaendelea na shuguli nyingine.
Haya bwana mtaka cha uvunguni.
 
chatts55 unaziona buku kumi ndogo? hayo masaa 9 kwenda dsm! mmh! Labda prof mchome atabadili mambo mbofumbofu ya wizara ya elimu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…