Nafikiri kuanzisha kakiwanda kidogo cha kuchakata viungo vya chakuala mbavyo najua kwa wapishi wa mijini inakuwa ni ngumu sana kuviandaa

Joined
May 12, 2009
Posts
25
Reaction score
35
khabari za mchana wadau na vijana wote mlio wanachama wa Jamii Forum pendwa kabisa. Napenda kuwakia jumatatu njema na yenye baraka kwa wote.

Nadhani inafahamika kama kwa sas kuna changamoto kidogo ya ajira ingawa tunasisitiziwa sana kuanzisha viwanda kwa ajili ya kufikia lengo la serikali tukufu ya awamu ya tano. Katika kufikia maazimio hayo nami nafikiri kuanzisha kakiwanda kidogo cha kuchakata viungo vya chakuala mbavyo najua kwa wapishi wa mijini inakuwa ni ngumu sana kuviandaa kwa wakati kutokana na kuwa na muda mfupi wawapo jikoni kutokana na harakati za kusaka pesa

Swali langu , je ni taratibu gani ambazo natakiwa nizifuate kabla ya kuanzisha hicho kiwanda kidogo na ni mamlaka gani ambazo natakiwa kudeal nazo awali ili niweze kupata idhibati na kuunga mkono harakati za Muheshimiwa?

Na kama kuna mwengine ambaye ana wazo zuri lakibiashara ambalo halihitaji mtaji mkubwa tunaweza tukabadilishana na wengine kwa ajili ya kutoa uzoefu kwa vijana ambao wanamaliza karibuni vyuo na kurudi kwenye elimu mtaa isiyo na cheti wala nini
 
Mambo yanayohusu usindikaji wa vyakula TBS,TFDA na SIDO lazima wahusike.
Anzia sido peleka wazo lako watakupa majibu mazuri kabla ya vibali..
Waje kukagua eneo kama linafaa kiafya kwa usindikaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…