Nafikiri kubadili jina; nitawavunjia heshima wazazi nikifanya hivyo?

Nafikiri kubadili jina; nitawavunjia heshima wazazi nikifanya hivyo?

Fisher_8

Member
Joined
Jul 26, 2019
Posts
80
Reaction score
225
Salamu kwenu,

Hivi wakuu itakuwa nawavunjia heshima wazazi nikiamua kubadili jina? Mzee alikwishaga tangulia mbele za haki, kabaki mama tu.

Kipindi cha zamani hata wakati baba yupo mama aliwahi nigusia kuwa jina nililopewa yeye wala alikuwa hakilipenda ila ni vile mzee alishalipangaga hata kabla sijazaliwa.

Nikiri hata mimi binafsi jina nililopewa silipendi pia ingawa ni la kinabii. Nataka kufuata taratibu nilibadili. Na ukizingatia bado kitambulisho cha utaifa sina.

Pia cheti cha kuzaliwa sina. Nilitaka mchakato niuanzie wakati nafatilia hivyo vitu.
 
Salamu kwenu.

Hivi wakuu itakuwa nawavunjia heshima wazazi nikiamua kubadili jina? Mzee alikwishaga tangulia mbele za haki, kabaki mama tu. Kipindi cha zamani hata wakati baba yupo mama aliwahi nigusia kuwa jina nililopewa yeye wala alikuwa hakilipenda ila ni vile mzee alishalipangaga hata kabla sijazaliwa.
Nikiri hata mimi binafsi jina nililopewa silipendi pia ingawa ni la kinabii. Nataka kufuata taratibu nilibadili. Na ukizingatia bado kitambulisho cha utaifa sina. Pia chetibcha kuzaliwa sina. Nilitaka mchakato niuanzie wakati nafatilia hivyo vitu.
Ni maamuzi yako mkuu, japo hoja ya msingi sijaona.
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Kuna majina yanaumba, unasikia mtu anaitwa
  • Matatizo
  • Shida
  • Sikujua
  • Taabu
  • Mahangaiko
  • Mateso
 
Kwa hiyo unataka utambulike rasmi kama Fisher au Fishclub?
 
Kuna majina yanaumba, unasikia mtu anaitwa
  • Matatizo
  • Shida
  • Sikujua
  • Taabu
  • Mahangaiko
  • Mateso
Kama alipewa jina linalofanana na haya hata mimi namuunga mkono abadilishe.

Jina lina uhusiano na Maisha ya mtu. Ukiitwa Shida/ Matatizo maisha yako yanakuwa na vipindi vichache vya furaha.
 
Badili tena haraka sana. usichelewe!! Hasa km aliyekupa hilo jina hakukupenda!! Au hakumpenda mama yako!!
Je aliyekupa jina hilo una mfeel vipi? Vizuri au vibaya...
Jamii unayoishi nayo ina mtazamo upi kwa maisha yako?

Wachawi hasa ndugu huroga sana kwa kutumia majina yako kamili....unazikwa makaburini...wazaramo wanasema mchawi ndugu...Ogopa sana ndg kimbiaaaaa!!! Mke/mme mchawi....

Kila ukiitwa hilo jina drsni zero za kutosha zina kuhusu....

Mama yako msikilize....ana jambo
 
Salamu kwenu,

Hivi wakuu itakuwa nawavunjia heshima wazazi nikiamua kubadili jina? Mzee alikwishaga tangulia mbele za haki, kabaki mama tu.

Kipindi cha zamani hata wakati baba yupo mama aliwahi nigusia kuwa jina nililopewa yeye wala alikuwa hakilipenda ila ni vile mzee alishalipangaga hata kabla sijazaliwa.

Nikiri hata mimi binafsi jina nililopewa silipendi pia ingawa ni la kinabii. Nataka kufuata taratibu nilibadili. Na ukizingatia bado kitambulisho cha utaifa sina.

Pia cheti cha kuzaliwa sina. Nilitaka mchakato niuanzie wakati nafatilia hivyo vitu.
Bila shaka ulifanikiwa!
 
Back
Top Bottom